Serikali ya 'mahustlers', kujaza mamilionea katika nyadhfa za baraza la mawaziri Kenya - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 18, 2022

Serikali ya 'mahustlers', kujaza mamilionea katika nyadhfa za baraza la mawaziri Kenya



CHANZO BBC SWAHILI

Viongozi walioteuliwa na rais William Ruto kujaza nafasi za baraza lake la mawiziri kwasasa wanapitia ukaguzi bungeni  kabla ya kuthibitishwa au kukataliwa kuchukua nyadhfa hizo.

Kamati ya bunge kuhusu uteuzi wa nyadhfa muhimu serikali imekuwa ikifanya vikao vyake hadharani ambavyo vimekuwa vikipeperushwa hewani na runinga zote za Kenya .

Wateule hao wameulizwa maswali mengi kuhusu rekodi yao kwa umma, maadili na uelewa wa masuala yanayokabili nyadhfa wanazotarajiwa kuzijaza.

Katika swali la maadili ,kila aliyeteuliwa alihitajika kutangaza thamani ya mali anayomilkii hadharani.

Na kwasababu wakati wa kampeni Muungano wa Kenya Kwanza ulioongozwa na rais William Ruto ulifanya kampeni yake kwa maudhui ya kumvutia Hassler – watu wa kipato cha chini, Wakenya wengi walitaraji kwamba walioteuliwa kurithi nyadhfa hizo  miongoni mwao kungekuwa na akina mama mboga na waendesha bodaboda {watu wa kipato cha chini katika jamii}.

Hatahivyo cha kushangaza ni kwamba walioteuliwa ni mamilionea na mabilionea.

Hii hapa orodha ya wateule hao na jinsi Wakenya walivyopokea matangazo ya thamani ya mali wanazomiliki.

Musalia Mudavadi - Ksh.4 Billion

Waziri Mkuu mteule amehudumu katika utumishi wa umma kwa miaka 33. Aliteuliwa katika Baraza la Mawaziri mnamo 1989 baada ya kumrithi babake kama Mbunge wa Sabatia.

Mudavadi aliambia Bunge kuwa ana thamani ya Ksh4 bilioni. Utajiri wake ulikuwa wa mali isiyohamishika - akitaja mali yake ya Riverside Drive ambayo hapo awali ilikuwa mwenyeji wa Kituo cha Musalia Mudavadi.

Pia alithibitisha kuwa na hisa katika makampuni mbalimbali - ikiwa ni pamoja na kampuni ya kukodisha ndege ya ndani ambayo haikuwekwa wazi

Kiongozi huyo wa zamani wa Chama cha ANC pia anajulikana kuwa na nyumba Karen na nyumbani kwake Mululu, Kaunti ya Vihiga.

Hatahivyo ni thamani ya mali yake iliovutia hisia za Wakenya mitandaoni

Aden Barre Duale  - Ksh 851 Million

Waziri wa Ulinzi mteule aliliambia Bunge kwamba alikadiria thamani yake kuwa takriban Ksh851 milioni. Utajiri wake ulikuwa wa mali isiyohamishika ambapo anapata Ksh10 milioni katika mapato ya kukodisha - na mifugo. Duale aliambia bunge kuwa miongoni mwa mali zake ni mbuzi, ng'ombe na ngamia 231.

Duale amekuwa katika afisi ya utumishi wa umma tangu 2007 alipochaguliwa kuwa mbunge wa eneo  la Dujis. Pia alihudumu katika serikali kuu ya muungano kama Waziri Msaidizi katika Wizara ya Maendeleo ya Mifugo.

Mnamo 2013, Dujis iligawanywa katika maeneo bunge mawili huku Duale akichaguliwa kuwa Mbunge wa Garissa Township. Alishikilia nafasi hiyo hadi uteuzi wake wa Baraza la Mawaziri.

Pia aliwahi kuwa Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa - kati ya 2013 na 2020.

Je Wakenya walisemaje baada ya kutangaza tahmani ya mali yake ilioshirikisha mbuzi na ngamia

Justin Bedan Muturi    Ksh. 700 million

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi ambaye ameteuliwa na rais William Ruto kuchukua wadhfa wa mwansheria mkuu hakusazwa na Wakenya katika mitandao ya kijamii alipoambia  kamati ya uhakiki kuwa ana thamani ya Sh700 milioni.

Alionesha ukuaji wa utajiri wake zaidi ya maradufu kutoka kwa tamko la awali alilotoa mwaka jana.

Ufichuzi wa Bw Muturi, hata hivyo, unaonyesha kiasi kikubwa cha thamani yake kutokana na kile alichofichua mwaka jana alipotangaza hadharani nia yake ya kuwania kiti cha urais.

Mnamo Novemba 2021 wakati wa mazungumzo na umma, Bw Muturi alisema alikuwa na thamani ya Sh300 milioni. Aliendelea kusema mali yake nyingi ilipatikana kupitia mikopo ya benki na malipo ya watumishi wa umma kwa miaka 36.

Alfred Ng’ang’a Mutua   Ksh.420 million

Mteule huyu wa wadhfa wa wizara ya masuala ya kigeni alijipata mashakani pale alipotakiwa kutangaza umiliki wa hoteli yake katika eneo la mashariki baada ya kusema kwamba alikuwa na thamani ya ksh.420m.

 Mutua alibainisha kuwa utajiri wake ulikuwa hasa katika umiliki wake wa hoteli ikiwemo ile ya A&L iliyoko Machakos. Pia alithibitisha kumiliki baadhi ya vyumba na biashara nyingine ndogo ndogo ambazo hakuzitolea maelezo.

Kamati ya uhakiki ilisema bwana Mutua alikuwa na thamani ya ksh. 200milioni kabla ya kuwa gavana mwaka 2013.

Kabla ya kuwa Gavana wa Machakos, Mutua alikuwa msemaji wa serikali kuanzia 2004 hadi 2012 alipojiondoa na kujiunga na siasa.

Kithure Kindiki  ksh .544 milion

Mteule wa Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki Jumanne, Oktoba 18, alifichua kwamba ana thamani ya Ksh544 milioni.

 Akiwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Uteuzi kwa ajili ya kuhakiki Bungeni, Kindiki alibainisha utajiri unaotokana na vyanzo mbalimbali vya mapato.

Alitaja vyanzo vyake vya mapato, kuwa uwekezaji wake katika hisa na mali isiyohamishika.

No comments:

Post a Comment