RAIS SAMIA ASAINI MABADILIKO YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 2, 2022

RAIS SAMIA ASAINI MABADILIKO YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MAJI


Na Mwandishi wetu Dar-es-salaam 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesaini Sheria ya Marekebisho ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2022 (The Water Resources Management Act, 2022).

Taarifa hii imetokewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bungeni Dodoma jana tarehe 1 November, 2022.

Ikumbukwe tarehe 15 September, 2022 Bunge la lilipitisha Muswada huu wa Sheria ya Marekebisho ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2022.

Kupitishwa kwa sheria hii kutaimarisha Bodi za mabonde ya Maji katika kusimamia Rasilimali za Maji nchini vilevile kuimarisha uhifadhi wa Vyanzo vya Maji nchini ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa Maji majumbani na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Wadau mbalimbali wamempongeza Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa kutambua umuhimu wa utunzaji, uhifadhi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji wakieleza kwamba Muswada huu umekuja wakati sahihi ambapo kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya Maji ikiwa kiwango cha Rasilimali za Maji kiko palepale.

Aidha, Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amesema;
“Hii ni taarifa njema kwetu na ni alama kubwa katika sekta ya Maji katika eneo hili muhimu la Rasilimali za Maji ikiwa kwa kuelekea kwenye mageuzi ya kweli katika mustakhabali wa usimamizi wa utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya Maji ambayo ndio roho ya upatikanaji wa Maji, kwa dhati kabisa Wizara ya Maji Tunamshukuru Mhe Rais kwa kuandika historia hii.”

No comments:

Post a Comment