SHUJAA MAJALIWA NDANI YA BUNGE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 10, 2022

SHUJAA MAJALIWA NDANI YA BUNGE


Majaliwa Jackson, kijana aliyewezesha kuokolewa kwa watu 24 katika ajali ya ndege ya Precision Air katika Ziwa Victoria Novemba 6 mwaka huu leo amefika Bungeni jijini Dodoma kama mgeni.

Majaliwa ambaye amepokelewa na kuanza mafunzo katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Tanga, ikiwa ni kufatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo leo ni kwa mara yake ya kwanza kuingia Bungeni, na amefika na kukaa katika jukwaa wanapokaa wageni wa Spika wa Bunge.

Katika ajali hiyo, Majaliwa alifungua mlango wa ndege na kuwezesha baadhi ya abiria kutoka ndani ya ndege.

No comments:

Post a Comment