Ameyasema hayo leo tarehe 05 Novemba, 2022, wakati alipofanya ziara yake Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Lengo la ziara hii ni kutembelea na kukagua ofisi ya Mtaalamu wa Miradi wa Umoja wa Posta Duniani kwa Ukanda wa Afrika Mashariki zilizopo katika Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Katika ziara yake Bw. Muthusi, ameeleza kuwa Mashirika ya Posta Duniani yanapaswa kutumia fursa ya maendeleo ya kidigitali katika kuboresha huduma zake ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha, ametumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais wake Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kidigitali katika Tanzania huku ikilirahishia Shirika la Posta Tanzania kutoa huduma zake sambamba na mahitaji ya wananchi.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Maendeleo Bw. Mutua Muthusi, ametembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Bakari Jabiri, katika mazungumzo yao ameipongeza Mamlaka hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuwezesha Mawasiliano nchini hususani katika Sekta ya Posta.
Itakumbukwa kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Posta Tanzania imepewa heshima na Umoja wa Posta Duniani ya kuanzisha Ofisi za Umoja wa Posta Duniani kwa Ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na kutoa Mtaalamu wa Kuratibu Miradi kwa Ukanda huo (UPU Field Project Expert for East Africa Sub-Region).
No comments:
Post a Comment