AFISA MTENDAJI WA KATA YA LIONJA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA RUSHWA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, September 21, 2025

AFISA MTENDAJI WA KATA YA LIONJA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA RUSHWA.



NA MWANDISHI WETU _ LINDI


Mnamo Septemba 18, 2025 katika mahakama ya wilaya ya Nachingwea limefunguliwa shauri la Uhujumu Uchumi namba 22689/2025 mbele ya Hakimu Mwandamizi Mkuu Mh.J.Mnguto, Jamhuri dhidi Seleman Ajibu Chimogo ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Lionja halmashauri ya wilaya ya Nachingwea.


Mshitakiwa amefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya Uchepuzi kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329, marejeo ya mwaka 2023 ikisomwa pamoja na Aya ya 21,Jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2)cha Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 marejeo ya mwaka 2023.


Mshitakiwa akiwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Lionja ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kwa makusudi alichepusha tani tano (5) za shehena ya mahindi ya bei nafuu (Tshs 700 kwa kilo) mali ya Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na kumuuzia Mfanyabiara kinyume na utaratibu. Walengwa wa mahindi hayo walikuwa ni wananchi wa kawaida kwa matumizi ya chakula na si bihashara.


Mshitakiwa amekana shitaka na yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Shauri hilo linakuja tena Oktoba 09, 2025.


Shauri hili limefunguliwa na Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Lindi Bw. Amandusy Mapunda.


TAKUKURU Lindi, Septemba 20, 2025.

No comments:

Post a Comment