Na Mwandishi wetu Mpwapwa
Hayo yamebainishwa na shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA), mkoa wa Dodoma Katika Kongamano lililofanyika wilayani mpwapwa lililojadili haki na changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu Katika upatikanaji wa taarifa.
"Ushirikishwaji mdogo bado ni kikwazi kwa watu wenye ulemavu kwenye vyombo mbalimbali vya maamuzi kuanzia ngazi za vijiji, mitaa Hadi halmashauri za wilaya, ili kuweza kubainisha mahitaji ya watu wenye ulemavu, wanatakiwa kushirikishwa ipasavyo" alisema Justus Mwantalimo, Katibu wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma.
Kwa upande wake Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime, amesisitiza umuhimu wa viongozi wa mitaa na polisi kata Katika kuwatambua watu wenye ulemavu.
"Niwaombe viongozi wa serikali za mitaa kwa pamoja ndani ya mkoa wetu wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla na Polisi kata, mshirikiane kuwatambua watu wanaoishi na ulemavu, tuwajue, tuwasemee, tuwakinge na kuwapa fursa ambazo zimeshaandaliwa na serikali" alisema Misime.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Josephat Maganga, ametoa wito kwa watu binafsi, mashirika ya umma, asasi za kiraia, Taasisi za kidini, kwa ujumla waone haja ya kusaidia kundi hili maalum kwa kuwajengea mazingira wezeshi na kupata mahitaji yao ya Msingi kwenye maeneo wanayoishi Katika hali ya usawa bila ubaguzi.
"Kuwatumisha Katika kuomba barabarani ni kuwaondolea utu wao, niwaombe wanaowatumia kupata maslahi yao binafsi kuacha Mara moja, tutimize wajibu wa kuwasaidia walemavu, ikiwa ni sehemu ya kuenzi Mila na desturi zetu za kuwajali wahitaji na wajibu wetu wa kijamii", alisema Maganga.
Maganga amezisisitiza familia, jamii na mamalaka ya Serikali za mitaa kuendelea kutoa matunzo na ulinzi kwa watu wenye ulemavu wasiokuwa na uwezo wa kujimudu badala ya kuwatumia Kama vitegauchumi kwa kuomba mitaani kuacha tabia hiyo.
Pia, SHIVYAWATA imeiomba serikali kutenga asilimia 10 ya maeneo kwa ajili ya biashara kwa watu wenye ulemavu, kuboresha huduma kutokana na ukosefu wa wakarimani wa lugha za alama Katika idara za serikali na kutengwa bajeti toshelezi ya Elimu kwa shule zenye watoto wenye mahitaji maalum.
Mbali na changamoto hizi Mwantalimo amesema Katika kipindi Cha mwaka mmoja SHIVYAWATA imefanikiwa kugawa vifaa saidizi na kuwaunganishwa watu wenye ulemavu na vyama vya watu wenye ulemavu mkoani Dodoma na kuwa na sauti moja.
No comments:
Post a Comment