Na Gideon Gregory - Kagera
Kwa upande wa wenyeji wa mchezo huo kupitia kwa kocha wao mkuu Mecky Maxime amesema kuwa anajuwa wanakwenda kucheza na timu ambayo iko vizuri na wanamichezo migumu nyumbani ambayo ni hiyo ya kesho dhidi ya Simba na nyingine watachuano na wachimba madini kutoka Mkoani Geita, Geita Gold hiyo ni michezo inayo waumiza kichwa.
“Kikubwa kesho wachezaji wangu wafuate yale nitakayo waelekeza na naamini kwa uwezo wa mwenyezi Mungu tutapata alama tatu,”amesema Mexime
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzie Ally Nasoro (Ufudu), amesema kuwa wao kama wachezaji wamejiandaa vizuri kwaajili ya mchezo huo dhidi ya Simba na mwalimu amefanyia marekebisho makosa yote yaliyo jitokeza katika mchezo ulio pita dhidi ya Azam.
Naye kaimu kocha mkuu wa Wekundu wa Msimbazi Simba Juma Mgunda amesema wamekuja Kagera kwaajili ya kushinda na Kagera Sugar na kuongeza kuwa hakuna mchezo mwepesi na michezo yote ni migumu kwa sababu hayo ni mashindano ya NBC Primer League.
“Moja ya kanuni ya fair play ni kumuheshimu mpinzani wako, kwahiyo sisi tunawaheshimu sana Kagera Sugar kwasababu ni moja kati ya timu nzuri,”amesema.
Pia kwa upande wake Nasoro Kapama mchezaji wa zamani wa walima miwa hao kutoka kanda ya Ziwa amesema wamekwenda Bukoba kuchukua alama tatu muhimu.
Kagera Sugar wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 dhidi ya wana ramba ramba wa Azam FC katika uwanja huo wa Kaitaba wakiwa nafasi ya Sita katika msimo wa ligi kuu na kujikusanyia jumla ya alama 22.
Huku wapinzani wao Simba wakiwa wana kumbukumbu ya kuibuka na ushindi mnono wa goli 5-0 dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na kushika nafasi ya pili wakiwa na alama 37, alama 4 nyuma ya mabingwa watetezi Young Africans wenye alama 41.
No comments:
Post a Comment