SEMINA YA KUJENGA UELEWA JUU YA UPUNGUZAJI WA MADHARA YA MAAFA YAFUNGULIWA DAR-ES-SALAAM - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, December 8, 2022

SEMINA YA KUJENGA UELEWA JUU YA UPUNGUZAJI WA MADHARA YA MAAFA YAFUNGULIWA DAR-ES-SALAAM

Afisa Tawala Wilaya ya Kinondoni Bi.Editha S.Elias akizungumza wakati akifungua Semina ya kujenga uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii iliyoandaliwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Disemba 6,2022 Jijini Dar-es-salaam
Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (SBU) Dorothy Pantaleo akizungumza wakati Semina ya kujenga uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii iliyoandaliwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Disemba 6,2022 Jijini Dar-es-salaam
Sehemu ya Washiriki wa Semina ya kujenga uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii iliyoandaliwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Disemba 6,2022 Jijini Dar-es-salaam
Sehemu ya Washiriki wa Semina ya kujenga uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii iliyoandaliwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Disemba 6,2022 Jijini Dar-es-salaam

Na Mwandishi wetu Dar-es-salaam

Afisa Tawala Wilaya ya Kinondoni Bi.Editha S.Elias amefungua Semina ya kujenga uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii iliyoandaliwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Disemba 6,2022 Jijini Dar-es-salaam

Lengo la Semina hiyo ni kuhakikisha kuwa Washiriki wanajengewa uelewa ili maďhara yanapotokea iwe rahisi kwa wananchi kuyakabili kutokana na uelewa ambao viongozi wao watapata kupitia Semina hiyo.

Aidha ,Bi.Editha amewataka washiriki wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu ili kutoka na tija ambapo kutokana na mafunzo watakayoyapata wafikishe kwenye jamii ili nao watambue namna ya kukabiliana na madhara ya maafa pindi yanapojitokeza.

Pia Afisa Tawala huyo ameipongeza ofisi ya Waziri Mkuu hasa ile Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kuendelea kutoa Semina hizo kwani zinasaidia kuongeza uelewa kwa washiriki katika kukabiliana na madhara ya Maafa pindi yanapotokea.

Semina hiyo imewajumuisha Watendaji Kata,Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kwenye Upande wa Maafa makundi hayo yamepewa kipaombele kutokana na wao kuwa karibu hivyo watasaidia katika kuwaelimisha wananchi nao wapate mafunzo hayo.

Kwa upande wake Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (SBU) Dorothy Pantaleo akitoa mada katika Semina ya kujenga uwelewa juu ya upunguzaji wa Madhara ya Maafa katika Jamii amesema kuwa ni jukumu la kila mmoja aliyepata bahati ya kushiriki katika semina hiyo kuwa mabalozi wazuri kwa wengine ili nao wapate uelewa wa namna ya kukabiliana na madhara ya Maafa.




No comments:

Post a Comment