Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Ally Khamis Juma (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA Bw. Andrew Mkapa, mara baada ya ufunguzi wa Maonesho ya Saba ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania, tarehe 4 Desemba, 2022 kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhe. Juma amewata wataaam kutoka Wizara ya Uwekezaji, VIwanda na Biashara chini ya uratibu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), pamoja na Wizara ya Biashara ya Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, kukutana mapema na kujadili changamoto za Sheria ya Leseni za Viwanda ambayo kwa sasa imepitwa na wakati.
Hatua hiyo itawawezesha wataalam hao kuja na mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Leseni za Viwanda, ambayo ni ya Muungano, ili kwenda sambamba na mabadiliko ya kiuchumi pamoja na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia. |
No comments:
Post a Comment