VIONGOZI WA DINI, WAHIMIZWA KUWAKUMBUSHA WAUMINI WAO KUJALI KANUNI ZA AFYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, December 16, 2022

VIONGOZI WA DINI, WAHIMIZWA KUWAKUMBUSHA WAUMINI WAO KUJALI KANUNI ZA AFYA


Na Shua Ndereka-Morogoro

Viongozi wa dini mbalimbali mkoani Morogoro wamehimizwa kupitia nyumba za ibada kuwambusha waumini wao, kujali kanuni za afya na kuachana na imani potofu dhidi ya magonjwa Mbalimbali na yale ya mlipuko.

Hayo yalibainishwa na Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Morogoro Masumbuko Igembya katika mafunzo ya kamati ya msingi ya afya kwa ngazi ya jamii kwa viongozi wa dini yaliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro ili kuwajengea uelewa zaidi juu ya magonjwa hayo ikiwemo Ebola, Polio, Surua, COVID 19 na VVU.

Katika utoaji wa elimu ya uwelewa juu ya magonjwa hayo, Masumbuko alisema kuwa, ugonjwa wa Polio humtokea watoto walio chini ya umri wa miaka 15 kwa ghafla na husababisha ulemavu wa viungo hivyo baadhi ya wazazi au walezi amekuwa wakihusianisha imani potofu pindi mtoto anapokutwa na tatizo hilo badala ya kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi.

“Ugonjwa huu unasababisha kupooza na hatimaye kifo, Virusi vya polio huingia mwilini kwa njia ya mdomo, kwa kunywa maji au chakula ambacho kimechafuliwa na kinyesi kutoka kwa mtu aliyeambukizwa virusi hivyo. 

Alisema kuwa Ugonjwa huu wa Polio hauna tiba lakini unaweza kuzuiliwa kwa kupata chanjo ya matone ya polio ambapo kampeni za utoaji wa chanzo dhidi ya ugonjwa huo tayari imetolewa kwa mizunguko mitatu na mzunguko wanne umefanyika mwishoni Novemba 2022.

Pia Masumbuko alibainisha ugonjwa mwingine wa Surua ambapo mkoani Morogoro iliripotiwa kuwa na wahisiwa wa ugonjwa huo 137, waliogundulika na ugonjwa huo watu sita, waliopona 136 na kifo kimoja.

 “Ugonjwa huu huzuilika kwa chanjo wanayopatiwa Watoto wenye umri wa chini ya miaka miwiliambao ufuatiliaji wa karibu wa wahisiwa wa ugonjwa huu unaendelea kufanyika kila siku katika vituo vya kutolea huduma na ngazi ya jamii pia kwa kutumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii”. Alisema Masumbuko

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kusirye Ukio aliisisitiza jamii kuepuka kucheza na nyani, sokwe, ama kula zao ama nyama ya wanyama pori ambayo haijaiva vizuri na kutoshiriki katika msiba au desturi za maziko zinazohitaji ugusaji wa maiti kama kuna mlipuko wa Ebola.

Mchungaji Lupakisyo Mwakasweswe wa kanisa la waadventista wa Sabato na Mkurugenzi wa huduma za vijana, Chaplensia na muziki kutoka jimbo la mashariki kati mwa Tanzania ECT ni miongoni mwa viongozi wa dini waliohudhuria mafunzo hayo ambapo alisema kuwa, wataalamu wa afya wamewakumbusha kuchukua taadhari na namna ya kudhibiti hivyo wanaendelea kuwatia moyo waumini kuendelea kuchukua tahadhari katika ugonjwa wa Ebola, na kupata chanjo ya UVIKO 19.

“Waumini tuweze kuchukua tahadhari juu ya surua na chanjo yake ni ya muhimu sana pia juu ya VVU ugonjwa upo na tuchukue tahadhari uaminifu kwa kufuata sheria ya Mungu na hii ndiyo halisi na hiyo ndiyo inayoweza kutuepusha na magonjwa mabaya yanayoua, licha ya kuwa wataalamu wamekuja na ufumbuzi wa dawa za kurefusha maisha. na tuepuke unyanyapaa kwa ugonjwa wa Ukimwi unaweza kuambukizwa si kwa zinaa pekee. Alisema Mchungaji Mwakaswewe.

Sambamba na hayo katika ufunguzi wa mafunzo hayo, yaliyofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatuma Mwasa aliwasisitiza pia viongozi wa dini kuhubiri amani na wafugaji kuachana na vurugu ziazopelekea uvunjifu wa amani katika maeneo mbalimbali mkoani humo na namna ya kuhimili ukame uliojitokeza kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

No comments:

Post a Comment