Na Mwandishi wetu Kagera
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Mhe. Toba Nguvila amewataka wavuvi mkaoni kagera kuyatumia mafunzo waliyopewa kwa ufasaha ili kuokoa maisha yao na yawengine.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Kuimarisha Ujuzi na Uzalendo kwa Vikundi vya Maokozi kwa Wavuvi katika Bahari na Maziwa Makuu yaliyoandaliwa na kuratibiwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu amemuagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Muleba kuhakikisha mafunzo haya yanaendelezwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Kemilembe Lwoza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Uongozi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mafunzo waliyoyatoa na kuwasihi wavuvi kuvitunza vifaa walivyopewa endapo ikibainika upotevu basi hatua za kisheria zitachukuliwa kwa upotevu huo.
Mafunzo ya Ujuzi na Uzalendo kwa Vikundi vya Maokozi kwa Wavuvi katika Bahari na Maziwa Makuu yaliyoandaliwa na kuratibiwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu yaliyoanza Novemba 28,2022 na kuhitimishwa Disemba 4, 2022 Mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment