Na Okuly Julius-Dodoma
Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi imetangaza matokeo ya mitihani ya 25 ya bodi hiyo iliyofanyika Nchi nzima kuanzia Novemba 22 Hadi Novemba 25,2022 ambapo katika matokeo hayo watahiniwa wapatao 48 wamefeli huku watahiniwa 474 wametakiwa kurudia baadhi ya mitihani kulingana na idadi ya masomo waliyofeli.
Akitangaza matokeo hayo Leo Januari 19,2023 Jijini Dodoma Mkurungenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi Godfred Mbanyi amesema jumla ya watahiniwa wapatao 1,216 walisajajiliwa ambapo watahiniwa 1,135 ndio waliofanya mitihani hiyo kati ya hao watahiniwa 613 wamefaulu na watahiniwa 474 wamefeli baadhi ya masomo na wamepewa fursa ya kurudia mitihani kulingana na idadi ya masomo waliyofeli
Sambamba na idadi hiyo watainiwa hao waliofeli ambao watarudia mitihani yao kulinaga na idadi ya masomo walifeli Mbanyi amesema wapo watahiniwa wengine 48 wamefeli masomo yote waliyofanya katika ngazi mbalimbali
"Watahiniwa 48 hawa wenyewe wamefeli kabisa mitihani yao kwahiyo wanapaswa kurudia zile ngazi za mitihani walizokuwa wamefanya"amesema Godfred Mbanyi
Aidha Mbanyi ameeleza sababu za kufeli watahiniwa hao ambapo amebainisha kuwa zimesababishwa na masomo ambayo yamejikita kwenye Hesabu.
Pia Mbanyi amebainisha kuwa bodi hiyo imeanza kujipanga kuanza kutumia mtaala mpya ifikapo Novemba 2023, hivyo amewashauri vituo navyuo vinavyofundisha masomo yanayohusiana na fani ya ununuzi na ugavi kuanza kuwaandaa wanafunzi wao kwa kuzingatia matakwa ya Mtaala mpya.
"Kutokana na mabadiliko ya Mtaala ,Bodi imetoa fursa kwa watahiniwa wote waliokuwa na masomo ya kurudia kutumia fursa hii kukamilisha masomo yao," amesema Mbanyi
Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ilianzishwa mwaka 2007 na Sheria ya Bunge Namba 23 ikiwa ina jukumu la kusimamia viwango vya kitaalamu na maadili ya wataalamu katika nyanja za manunuzi na vifaa.
No comments:
Post a Comment