MSIFANYE KAZI KWA MAZOEA JIKITENI KATIKA KUTATUA KERO ZA WANANCHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 19, 2023

MSIFANYE KAZI KWA MAZOEA JIKITENI KATIKA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene akihutubia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Shughuli za Serikali yaliyofanyika Ukumbi wa Ofiai za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dodoma Januari 19, 2023.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi katika Mafunzo ya kujenga Uwezo kuhusu kuhusu Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Shughuli za Serikali kwa Menejimenti ya Ofisi hiyo na baadhi ya Maafisa wa Ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Menejimenti ya ofisi yake mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo yao ya Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini yaliyofanyika Dodoma.
Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika mafunzo ya kujenga uwezo na uelewa namna Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Shughuli za Serikalini.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na Okuly Julius-Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu GEORGE SIMBACHAWENE ameitaka Idara mpya ya ufuatiliaji na tathmini iliyopo ofisi ya Waziri Mkuu kuimarisha uwajibikaji kwa kuhakikisha majukumu yao yanalenga kutatua kero za wananchi ili kuleta matokeo chanya yenye ufanisi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Januari 19,2023 ,Jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Idara ya ufuatiliaji na tathmini ya utendaji wa shughuli za Serikali ambapo amesema Ofisi hiyo ni kungo katika kutekeleza shughuliza Serikali na kuboresha huduma za Wananchi.

"Mafunzo haya yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili yatumike vizuri kutafakari mafanikio, changamoto na kuweka mikakati itakayoboresha utendaji unaozingatia matokeo,

Na kuongeza kuwa "tafakari hiyo ijikite katika kuangalia ufikiwaji wa malengo ya kitaifa kwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano unaotekelezwa kuanzia mwaka 2021/22-2025/26; Mwelekeo wa Sera za Chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2020 2030; Dira na Dhima ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kifikia malengo ya kitaifa na kuboresha hali za maisha ya watu,"Amesisitiza Simbachawene

Waziri huyo amesema kuwa Maafunzo hayo yanatarajiwa kuwa na chachu ya kuimarisha uratibu wa shughuli za Serikali (Coordinated Government) ambao utasaidia kuongeza ufanisi na tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Katika hili sina wasiwasi kwa sababu Wataalam walioalikwa kutoa mada katika Mkutano huu ni wabobezi katika maeneo haya kwa maana ya uzoefu walionao katika utekelezaji wa shughuli za Serikali,"Amesema Simbachawene


Katika hatua nyingine,Waziri huyo ameelekeza kuwa matokeo ya mafunzo hayo yatumike kufanya uratibu na usimamizi katika kupima na kufanya tathmini ya utendaji kazi.

Pia Simbachawene amesema kuwa uwekwe utaratibu ambao utawezesha uchambuzi wa Taarifa za kisekta na kutoa mrejesho wa maeneo yanayohitaji kuboreshwa au kupewa msukumo zaidi.

"Kwa sasa hili halifanyiki vizuri, hivyo Idara mpya ya Ufuatiliaji na Tathmini isimamie hili na kuhakikisha kunakuwa na mrejesho kwa Wizara na Taasisi zote ili kuimarisha uwajibikaji,

Na kuongeza kuwa "Taarifa ya utendaji wa Serikali iwasilishwe na kujadiliwa katika vikao kazi vya Baraza la Mawaziri kila robo mwaka. Utaratibu wa sasa wa kila Wizara kuwasilisha Taarifa yake kwenye vikao hivyo unaondoa dhana ya uratibu. Taarifa ijikite katika utekelezaji wa masuala ya kisera na kimkakati ili kuona mwenendo wa utekelezaji wa shughuli za Serikali," amesisitiza Simbachawene

Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.JOHN JINGU amesema watatekeleza majukumuyao kwa matokeo makubwa na kwa ufanisi ili kumsaidia Waziri Mkuu na Rais katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment