HOSPITALI YA WILAYA YA ITILIMA YAANZA KUTOA HUDUMA ZA UPASUAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 16, 2023

HOSPITALI YA WILAYA YA ITILIMA YAANZA KUTOA HUDUMA ZA UPASUAJI


OR-TAMISEMI

Hospitali ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu imeanza kutoa huduma za upasuaji kwa wakinamama wanaopata uchungu pingamizi.


Akizungumza Mganga mkuu wa Wilaya ya Itilima Dkt. Anold Musiba amesema “Tumefanimiwa kuanza kutoa huduma ya upasuaji kwa kina Mama wajawazito wanoshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida kutokana na sababu mbali mbali pia tumeanzisha huduma ya watoto njiti pamoja na wale wanaohitaji uangalizi wa karibu sana baada ya kuzaliwa(NICU)”.

Pia Dkt. Anold Musiba ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwanamna inavyojitoa kuhakikisha huduma bora za afya zinawafikia watanzania wote kokote kule waliko.

No comments:

Post a Comment