MAKUMI YA WANAFUNZI WAKIMBIZWA HOSPITALINI BAADA YA KULA NYAMA YA NYOKA SHULENI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, January 13, 2023

MAKUMI YA WANAFUNZI WAKIMBIZWA HOSPITALINI BAADA YA KULA NYAMA YA NYOKA SHULENI

Wanafunzi kadhaa walilazwa hospitalini Jumatatu, Januari 9, alasiri baada ya kula chakula chao cha mchana kilichotolewa na serikali.

Wanafunzi hao wa Shule ya Msingi ya Mandalpur, wanaripotiwa kuathirika baada ya kula chakula hicho kilichokuwa na nyama ya nyoka.

Maafisa walisema kuwa takriban wanafunzi 20 kati ya 53 waliokuwepo shuleni wakati huo, walikula chakula hicho. 

Habari hizo zilipoenea mtaani, wanakijiji wenye hasira walikusanyika shuleni humo na kuharibu gari la mwalimu mkuu Wanafunzi kadhaa walilazwa hospitalini Jumatatu, Januari 9, alasiri baada ya kula chakula chao cha mchana kilichotolewa na serikali. 


Lakini kulikuwa na hofu baada ya mfanyakazi wa shule hiyo aliyepika chakula cha mchana kudai kuwa nyoka alipatikana kwenye chombo kimoja kilichokuwa na pojo. 

"Watoto wote walikimbizwa mara moja katika Hospitali ya Rampurhat baada ya kuugua.Wanawake wawili waliokuwa wanapika walimwona nyoka walipokuwa wakipakuwa dengu. Mmoja wao au wawili walikuwa wameiweka tu kinywani mwao." 

"Baada ya kumuona nyoka huyo, kila mtu aliombwa aache kula," mwalimu mkuu Nimai Chandra Dey alisema. 

Habari hizo zilipoenea mtaani, wanakijiji wenye hasira walikusanyika shuleni humo na kuharibu gari la mwalimu mkuu. Wanafunzi hao waliruhisiwa kwenda nyumbani baada ya kutibiwa na wako katika hali sawa kiafya. 

     Chanzo ni TUKO.co.ke

No comments:

Post a Comment