Na Okuly Julius-Dodoma
Dkt.Mganga ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya program ya Serikali ya SHULE BORA kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika Januari 27,2023 wilayani Kondoa.
Mradi wa Shule Bora ni Programu ya Serikali Tanzania,ikifadhiliwa na Serikali ya Uingereza kwa lengo la kuinua ubora wa elimu ya Awali na Msingi katika mikoa tisa (9) hapa nchini kwa ushauri elekezi kutoka Cambridge Education ikishirikiana na mashirika ya ADD International, International Rescue Committee na Plan International.
"Mradi huu wa Shule Bora unatupa nguvu na matumaini makubwa kama mkoa kuona kuwa tunaweza kufikia malengo yetu angalu kuongeza ufaulu kwa asili 95 ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba na angalau asilimia 75 ya wanafunzi wanaohitimu kidato Cha Nne Wawe na ufaulu wa daraja la 1-3,"amesema Dk.Mganga
Hata hivyo Katibu tawala huyo amesema kuwa swala la Elimu katika Mkoa wa Dodoma bado halijatangazwa vizuri na kuwataka waandishi wa habari wakawe chachu katika kuielimisha jamii kuwa wanajukumu la kushiriki kikamilifu katika kuboresha elimu.
"Naamini mara baada ya kumalizika kwa mafunzo haya mtakwenda kuifungua jamii kifikra kuwa wana jukumu la kushiriki katika kuinua ubora wa elimu katika Mkoa wetu na naomba sana kwenu waandishi mwaka huu Dodoma tumebeba agenda yetu ya sekta ya elimu hivyo kupitia nyinyi tunaamini itafanikiwa kwani nyinyi mkiamua kutumia vyombo vyenu vizuri hakuna kitakachoshindikana,"ameongeza Dkt.Mganga
Ambapo Dkt.Mganga ameeleza kuwa kwa sasa mkoa wa Dodoma una upungufu wa vyumba vya Madarasa zaidi ya 7000 ndipo akapeleka ombi kwa wazazi na jamii kwa ujumla kujikita katika kuhakikisha kila mwaka katika gitongoji,kata na mitaa yao wanaweza kujenga angalau chumba kimoja cha darasa ili kuwasaidia watoto wenye umri wa kwenda shule kuanza masomo.
Dkt.Mganga amesema kuwa Mwaka huu peke yake zaidi ya wanafunzi elfu 90 wanatarajiwa kuanza masomo ambapo Mpaka kufikia January 26.2023 asilimia 89.7 ya wanafunzi wa darasa la awali walioripoti shule,huku asilimia 94.2 Kwa darasa la kwanza na asilimia 66.95 kidato Cha kwanza wakiwa wameripoti shule.
Naye Mratibu wa Program ya SHULE BORA Mkoa wa Dodoma Mtemi Zombwe amesema kuwa ili kufanikisha mchakato wa kuinua na kuboresha elimu ni vyema kila mmoja akatambua kuwa anajukumu la kushiriki katika mchakato huo.
"Mradi wa SHULE BORA ni Programu mahususi kabisa kwa ajili ya kuinua na kuboresha ubora wa elimu hivyo ili tufaniliwe ni lazima kila mmoja ajue ana wajibu wa kuhakikisha elimu inakuwa bora,"
Na kuongeza kuwa "Wazazi au jamii kwa ujumla ni lazima washirikiane na Serikali ama walimu katika masuala mbalimbali ikiwemo kuhakikisha miundombinu inaborshwa kwa upande wa kujifunzia,kufundishia alafu pia iwe Jumuishi pamoja na luhakikisha mifumo ya elimu inaimarishwa kwa hapo tutakuwa tunaboresha na kuinua elimu yetu kila mmoja ashiriki,"Amema Zombwe
Zombwe ametoa wito kwa wandishi wa habari kufanya kazi ya kuhamasisha,kuelimisha na kuhabarisha jamii juu ya Mradi wa SHULE BORA na kwa namna gani inachochea ubora wa elimu hapa nchini.
Mratibu huyo amebainisha kuwa katika ngazi ya kitaifa SHULE BORA itatoa pia msaada wa kiufundi kwa serikali ya Tanzania, pamoja na utekelezaji wa mradi wa pili wa LIPWA KWA MATOKEO yaani Education Program for Results Two.
"Mradi unalenga kuwa na matokeo makubwa na endelevu katika elimu ,kwa kusaidia kuanzisha na kuimarisha mifumo na taratibu za elimu ,kwa kufanya hivyo ,mpango utaimarisha matokeo ya ujifunzaji,hususani katika KKK na kiwango cha wanafunzi kusailia shule,"amesema Zombwe
Mradi wa SHULE BORA utatekelezwa katika mikio 9 ikiwemo Dodoma,Mara,Katavi,Rukwa,Kigoma,Singida,Simiyu,Pwani na Tanga hadi ifikapo mwaka 2027 kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK aid kwa gharama ya poundi za Kiingereza milion 89 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 271.
No comments:
Post a Comment