KILELE CHA MIAKA 59 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR TUTAADHIMISHA KWA KUPANDA MITI WANANCHI TUJITOKEZE-DKT.JAFO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 9, 2023

KILELE CHA MIAKA 59 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR TUTAADHIMISHA KWA KUPANDA MITI WANANCHI TUJITOKEZE-DKT.JAFO


Na Gideon Gregory, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Dkt. Selemani Jafo ametoa rai kwa wakazi wa Jiji la Dodoma, wadau mbalimbali na waandishi wa habari kumuunga mkono Makamu wa Rais na viongozi wengine katika shughuli za upandaji wa miti siku ya kilele cha miaka 59 ya Mapinduzi matakufu ya Zanzibar.

Rai hiyo ameitoa katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika leo Januari 9,2023 Jijini Dodoma kuhusu maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayo fanyika Januari 12 mwaka huu.

Waziri Dkt. Jafo amesema mwaka huu hakutokuwa na sherehe kubwa za maadhimisho ya Mapinduzi katika uwanja wa Amani kama ilivyo zoeleka, baadala yake gharama zilizopangwa kutumika katika Sherehe hizo zitaelekezwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo hususani sekta ya elimu ikiwemo kuongeza madarasa, madawati na maabara.


“Maadhimisho haya yatahusisha ukaguzi na uzinduzi wa miradi ya maendeleo na uwekezaji katika sekta mbalimbali chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,”amesema Dkt.Jafo

Aidha ameongeza kuwa katika kuadhimisha maadhimisho hayo Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imeazimia kuendeleza shughuli za upandaji miti katika viunga na maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma.

“Tarehe 12 Januari siku ya kilele cha maadhimisho haya makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango atawaongoza wananchi wa Jiji la Dodoma kupanda miti katika barabara ya Dodoma - Dar es salaam kuanzia stendi kuu ( Nane nane) hadi Ihumwa na shule ya msingi Msalato na huko pia ataongoza wananchi kupanda miti katika eneo hilo,”amesema Dkt.Jafo


Kila mwaka Serika ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huadhimisha na kuenzi Mapinduzi Matakufu ya Zanzibar yaliyotokea Januari 12,1964 ambapo utwala wa sultan uliondolewa na kutoa uhuru kamili kwa watu wa visiwani humo.

No comments:

Post a Comment