Na Mwandishi wetu Dar-es-salaam
Wanafunzi 26 kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wametembelea ofisi za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Wanafunzi hao wametembelea leo Januari 10, 2023 katika ofisi za BRELA Makao Makuu, Jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa BRELA, wamewaelimisha wafunzi hao namna haduma za sajili za kibiashara pamoja na utoaji wa lesini zinavyotolewa, huku wakiwasihi kuwa mabalozi katika kueneza elimu ya urasimishaji biashara hapa nchini.
BRELA imekuwa ikitoa elimu kwa makundi mbalimbali ya wanafunzi kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vikuu lengo likiwa ni kukuza uelewa wa wanafunzi kuhusu masuala ya urasimishaji biashara.
No comments:
Post a Comment