Waziri Bashe awataka wakulima kulinda namba zao za utambulisho wa mbolea za ruzuku - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 5, 2023

Waziri Bashe awataka wakulima kulinda namba zao za utambulisho wa mbolea za ruzuku


Na Mwandishi wetu Rukwa

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewataka wakulima waliojiandikisha kwenye mfumo wa ruzuku kuwa walinzi wa namba zao za siri na kutoa taarifa pindi wanapopata ujumbe wa kununua mbolea hizo wakati si kweli.

Waziri Bashe ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Januari, 2023 katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Ilemba, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

Amesema, imeibuka tabia za mawakala na watendaji wasiokuwa waaminifu kuhijumu juhudi za serikali za kuhakikisha wakulima wananufaika na mbolea za ruzuku kwa kutumia namba za wakulima kuscan mifuko ya mbolea bila mkulima mwenyewe kupokea mbolea hiyo.

"Mkipata ujumbe kwamba mmenunua mbolea wakati si kweli pigeni simu kwenye namba inayoonekana mwishoni mwa ujumbe huo na kutaoa taarifa", alisisitiza Waziri Bashe.


Aidha, Waziri Bashe amesema anatambua kuwa kijiji hicho hakina wakala wa mbolea na kuahidi kuwa jambo hilo linafanyiwa kazi na kuwahakikishia misimu ijayo ya kilimo wizara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) watafikisha wakala katika kijiji hicho.

"Tumetoa ruzuku za mbolea, najua huku hakuna kituo lakini wasambazaji wataweka kituo pale Lahela ili kuwawezesha kununua mbolea na kutosafiri umbali mrefu" Alisisitiza waziri Bashe.


Mwisho Waziri Bashe aliwasihi wakulima wa kijiji hicho kujiandikisha pindi wanapohitaji mbolea na kuwasilisha majina hayo ofisi ya kijiji watakaofanya mawasiliano na wakala ili waweze kuleta mbolea kulingana na mahitaji yao ambapo zitascaniwa hapohapo kijijini na kila mkulima aliyejiandikisha atapokea mbolea yake.

No comments:

Post a Comment