Na Okuly Julius Dodoma
Hayo yameelezwa leo Januari 5,2023 Jijini Dodoma kwenye kikao kazi cha wataalamu wa Wizara na Taasisi za Serikali kuhusu kujenga uelewa na kujadili namna bora ya kutekeleza maelezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo wa anwani za makazi.
Akizungumza kwenye kikao hicho ambacho pia kimejumuisha namna mfumo wa kidigitali wa anwani za makazi (NaPA)unavyofanya kazi, Mkurugenzi msaidi,wa utawala wa mawasiliano Suleiman Mvunye amesema
suala la anwani za makazi linapaswa kueleweka kuwa taarifa ya msingi katika kutoa na kupokea huduma bidhaa.
Amesema utekelezaji wa mfumo huo wa anwani za makazi unapaswa kutekelezwa kwa wakati ili kutambua wananchi wanaowahudumia na kuchochoea maendeleo.
"Sisi kama Wizara ni wasimamizi kwa niaba ya Serikali hivyo ni jukumu la Kila Mmoja wetu kufanya kazi kwa uadilifu kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa Kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto zote zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wake hatua ambayo itaimarisha usalama na utambuzi wa watu,"amesema Mvunye
Amesema,baada ya kikao hicho Wizara inatarajia utekelezaji wa kina kuanza mara moja kwa kuzingatia uendelezaji wa mfumo wa anwani za makazi ambao unazingatia uhifadhi na kutunzwa na watu wote.
"Kwa kufanya hivyo tutafanikiwa, sisi sote lazima tuungane kuhifadhi miundombinu yote hasa ikizingatiwa kuwa Serikali imetumia gharama kubwa ya bilioni 28 Katika kutekeleza mfumo huu unaohitajika kuwa endelevu kwa vizazi vijavyo,hivyo kila Wizara inapaswa kuwa mbele kuwezesha mfumo huu kwa kushirikiana na kuhamasisha wananchi,"amesisitiza Mvunye
Akitoa maelekezo kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu,Mratibu wa anwani za makazi kitaifa Jampyon Mbugi amesema Taasisi zote zinapaswa kuhakikisha taarifa ya anwani za makazi inakuwa taarifa ya msingi wakati wa kutoa na kupokea huduma kwa kujumuisha mifumo ya kielekroniki.
Aidha amesema Mifumo yote ya kutoa huduma inaelekezwa kufanya utaratibu wa kuunganishwa na mfumo wa anwani za makazi ili kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
"TANROADS na Tarura kwa kushirikiana na wadau wengine mnaelekezwa kuhakikisha mnaandaa mikakati ya kuendelea kuweka na kuunda nguzo zenye majina ya sehemu mnazozihudumia,"amesema Mbugi
No comments:
Post a Comment