CHUO CHA MAJI NDIO JKT YETU TUWATUMIE VIJANA WALE KUTATUA CHANGAMOTO-AWESO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 6, 2023

CHUO CHA MAJI NDIO JKT YETU TUWATUMIE VIJANA WALE KUTATUA CHANGAMOTO-AWESO


Na Okuly Julius-Dodoma 

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema wanajivunia ufanisi mkubwa kwenye utekekezaji wa miradi ya maji huku akiwataka watendaji kuekekeza nguvu kwenye utoaji huduma ili kuondoa malalamiko ya wananchi ikiwemo kubambikiwa bili za maji.


Mhe.Aweso ameyasema hayo wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa sekta ya maji leo Februari 6,2023 Mtumba Jijini Dodoma

Amesema kuwa upatikanaji wa maji mijini kuna kazi kubwa imefanyika sasa ni kwenda kuongeza nguvu kwenye utoaji wa huduma ili kuondoa malalamiko ya wananchi ikiwemo ya kubambikiwa bili za maji.

Waziri huyo Amewataka watendaji wa Mamlaka za maji kwenda kusimamia kikamilifu miradi ya maji ili kuwe na ufanisi na Wataalam kufanya tathimini zitakazosaidia viongozi kuifanya Maamuzi,ikiwemo pia eneo la uandaaji wa mikataba uzingatie maslahi ya serikali.


"Asilimia kubwa ya mikataba ikitokea changamoto atakayeshindwa ni serikali, mfano mradi was Same- Mwanga changamoto zake ziko kwenye karatasi
Ukitaka kufanya kazi kubwa na nzuri ifanye kama yako ,"

Na kuongeza kuwa "katika kipindi Cha miaka miwili mambo mengi yamefanyika na hivyo kuongeza idadi ya wananchi wanaopata Huduma ya maji," amesema Aweso


Hata hivyo amebainisha kuwa eneo la manunuzi bado lina malalamiko lazima walibebe na kulifanyia marekebisho.

Pia amewaagiza watendaji kuwatumia vijana kutoka Chuo Cha Maji kufanya mazoezi ya vitendo (field) ili waweze kuonesha utaalam wao na kusaidia changamoto mbalimbali.

Amewataka kutumia mkutano huo kufanya tathimini wapi Wizara ya Maji ilipotoka,, ilipo na inapokwenda.

"Maji hayana mbadala, maji ndio uhai mtu anapokosa.maji kelele zake mnazifahamu, maji ni siasa kila mtu anahitaji maji,"Chuo Cha maji ndio JKT ya Wizara ya Maji," amesisitiza Aweso



Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji MaryPrisca Mahundi amesema kuwa miradi mingi ya maji inatekekezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

"Hata yale malalamiko na manung'uniko yaliyokuwepo kutoka kwa wabunge siku hizi hayapo au yameisha kabisa, hilo linaonesha kazi kubwa imefanyika,"

"Tuendelee kufanya kazi kuhakikisha maji safi bombani yanawafikia wananchi wote," amesema Mahundi



Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maji Injinia Antony Sanga amewataka watendaji kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata Huduma bora za maji ya kutosheleza.

"Mambo ya kufanyia kazi ni pamoja na kwenda kuboresha uwajibikaji kukumbushana kama viongozi na watendaji, watumishi kuwa wabunifu , utendaji kazi wa kasi changamoto kubwa ni kasi hairidhishi" amesema Sanga


Pia akawataka watumishi hao kuacha kuvujisha siri za Ofisi na baaadhi ya wanaofanya hivyo ni watendaji wakuu.

Ámesema kuwa baadhi ya watendaji wamekuwa na maamuzi ya kibabe

"Kuna wengine Wana maamuzi ya kibabe nimeshakuambua hunifanyi kitu ,unyanyasaji ubinafsi, lugha chafu, Kauli za maudhi,watumishi wanavumilia lakini mwisho wa siku hawakusaidii," amesema Sanga

No comments:

Post a Comment