WAZIRI MKUU MSTAAFU JOHN MALECELA -TULINDE AMANI YETU KUKUZA SEKTA YA UTALII - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, April 11, 2026

WAZIRI MKUU MSTAAFU JOHN MALECELA -TULINDE AMANI YETU KUKUZA SEKTA YA UTALII




SAME.

MAKAMU wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, John Samuel Malecela amesema kuwa, swala la Utalii kokote Duniani linaenda sambamba na swala la Amani na Utulivu na kuwaomba wananchi kuhakikisha wanalinda Amani ili kukuza Utalii nchi na kuendelea kujinufaisha kupitia sekta hiyo.

Malecela alitoa kauli hiyo jana wakati wa Uzinduzi wa tamasha la Same Utalii festival lililofanyika katika viwanja vya stendi wilayani Same mkoani Kilimanjaro ambapo alisema kuwa, utalii ni kite ambacho huchangia kuleta fedha za kigeni.

Alisema kuwa, baadhi ya nchi ulimwenguni serikali zinaendeshwa kwa fedha za Utalii na kuwataka kulichukulia swala hilo kwa umakini mkubwa.

Kiongozi huyo alidai kuwa, misingi ya Utalii ni ukarimu kwa wageni na kuwataka wananchi wa wilaya ya Same kuwa mfano katika ukarimu ili kukuza Utalii wa wilaya ya Same.

"Hata sehemu kukiwa na njiwa 10,000 wamejaa lakini jiwe likigonga tu wote wanakimbia kwa hiyo na sisi utalii wetu uanze na sisi wenyewe Watanzania kuwa na Amani ni jambo la msingi sana kwani Amani ndio italeta na kuwakaribisha watalii na ndio itatufanya tuendelee kukua kiuchumi" Alisema Malecela.

Na kuongeza "Swala la ukarimu kwa wageni ni kitu muhimu sana mahali pengine watu hawaendi kwa sababu hakuna moyo wa kuwapokea wageni lakini kwetu same tuwe na moyo wa kuwapokea wageni ili kukuza utalii wetu".

Alisema kuwa, kinachotuunga pamoja ni Amani na kuwasihi Watanzania kuendelea kuitunga na mambo mengine yatafuata.

"Ili Utalii wa same uweze kukua ni lazima uanze na sisi wenyewe wanasama kuwa na moyo dhabiti wa ukarimu ili wanapokuja na kurudi wakatoe sifa ni kweli wataenda kuona wanyama lakini mkiwakaribisha kwa moyo upande hawatarudi tena" Alisema Malecela.








No comments:

Post a Comment