FUATILIENI TUHUMA ZINAZOWAKABILI WATENDAJI WA KATA -DKT.MPANGO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, February 14, 2023

FUATILIENI TUHUMA ZINAZOWAKABILI WATENDAJI WA KATA -DKT.MPANGO


Na Okuly Julius-Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kufuatilia tuhuma zinazowakabili watendaji wa kata ikiwemo kuwanyanyasa wananchi Katika utoaji huduma naikibainika hatua kali zichukuliwe.


Mpango ameyasema hayo Februari 14, 2023 Jijini Dodoma wakati wa Hafla ya kukabidhia magari kwa mameneja wa Mikoa na Wilaya wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Pikipiki kwa Watendaji wa kata.


Aidha ametala Pikipiki hizo kupelekwa kwenye kata zenye uhitaji na zilizopo pembezoni na kutoa wito kwa watendaji kuhakikisha zinatunzwa na kufanyiwa matengenezo kwa wakati ili ziendele kuleta maendeleo ya Nchi.

Mpango amesema wamekuwa wakipokea tuhuma nyingi huku akiwataka Wakurugenzi wote Nchini kufuatilia hatua stakihiki za kisheria na nidhamu kwenye tuhuma zinazopelekwa serikalini
Pia amewataka wakurugenzi wa halmashauri kutenga bajeti na kusimamia miradi ipasavyo.


Aidha amewataka watendaji hao kufanyakazi pasina kumwonea mtu na kusimamia sheria.
Katika hatua nyingine amewataka kutumia magari na pikipiki hizo kwa ajili yakuwatumikia wananchi na si kwamanufaa yao wenyewe.


Awali Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema jumla ya bilioni mbili zimetumika kununulia pikipiki 916 , Magari 54 yatagawiwa kwa mameneja wa mikoa na wilaya wa TARURA na kwakuanzia yatapelekwa pembezoni kwakuwa ndo kuna uhaba mkubwa wa Usafiri kwa watendaji katika kuwafikia wananchi katika utoaji huduma.


Naye Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo ametaka kufanyika kwa mapitio ya ukusanyaji wa kodi kati ya TAMISEMI na TARURA ili kuona wapi kwenye tija nakuweza kupewa jukumu hilo utaratibu wa ukusanyaji wa kodi.


Hata hivyo amesema kuwa kunahitajika muongozo wa mfumo wa upatikanaji wa mafuta kila mwezi pamoja na utaratibu utakaowafanya watendaji kupata matengenezo ya magari na pikipiki hizo ili kulinda mali za serikali.


No comments:

Post a Comment