KATIBU MKUU YAKUBU APOKEA RASMI OFISI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 17, 2023

KATIBU MKUU YAKUBU APOKEA RASMI OFISI


Na Shamimu Nyaki

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu leo Februari 17, 2023 Mtumba Dodoma amepokea rasmi Ofisi kutoka kwa Mtangulizi wake Dkt.Hassan Abbasi ambaye amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mara baada ya kupokea ofisi Katibu Mkuu Yakubu amemshukuru Katibu Mkuu Abbasi kwa kumuongoza vyema wakati akiwa Naibu Katibu Mkuu, ambapo amesema mazuri yote walioanzisha na mageuzi makubwa katika wizara hiyo atayaendeleza.


"Tunayo mengi mazuri ambayo tumeyatekeleza pamoja ikwemo kuanzisha Upatikanaji wa Vazi la Taifa, Mdundo wa Taifa, Kubidhaisha Kiswahili na ujenzi na uboreshaji wa miundombinu, niwahakikishie tutayakamikisha kwa wakati na kuyaendeleza" amesema Bw. Yakubu.

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi Ofisi Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amesema wizara hiyo ni wizara ambayo imekua ni miongoni mwa wizara zinazofanya vizuri Kwa sasa kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanyika.


Amesema kuwa, Sekta za Wizara hiyo zimekua nguvu shawishi kwa Taifa kwa kutoa furaha, huku akitaja mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja na kurejeshwa Kwa Tuzo za Muziki na Filamu, Kufufuliwa kwa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Kukamilisha hatua za ujenzi wa viwanja vya michezo na Sanaa jijini Dar es Salaam na Dodoma.

No comments:

Post a Comment