MHE.NDEJEMBI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUKERWA NA CHANGAMOTO ZA WANANCHI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, February 25, 2023

MHE.NDEJEMBI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUKERWA NA CHANGAMOTO ZA WANANCHI.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Deogratius Ndejembi,akizungumza leo Februari 25,2023,Jijini Dodoma , wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha Makatibu tawala wasaidizi na wakuu wa Idara katika mamlaka za serikali za mitaa.


Na Okuly Julius,Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Deogratius Ndejembi amewataka Makatibu tawala wasaidizi na wakuu wa Idara katika mamlaka za serikali za mtaa kukerwa na matatizo ya wananchi,kutatua kwa wakati changamoto zao,kupatikana kwa urahisi ofisini na kuondoa urasimu katika utendaji wao wa kazi.

Mhe.Ndejembi ameyasema hayo leo Februari 25,2023,Jijini Dodoma , wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha Makatibu tawala wasaidizi na wakuu wa Idara katika mamlaka za serikali za mitaa.


Pia Mhe.Ndejembi amewataka watumishi hao kujenga tabia ya kusikiliza na kutolea ufafanuzi matatizo ya wananchi na wasisubiri mpaka taarifa ziwafikie viongozi wa juu wakati nao wana uwezo wa kuyatatua na kuyatolewa majawabu.

"Sio lazima viongozi wa juu ndio watolee ufafanuzi malalamiko ya wananchi wakati nyinyi mpo na mnawajibu wa kufanya hivyo kabla hayajafika mbali na imani yangu ni kwamba mtakwenda kuyatumia mafunzo haya katika kutatua changamoto za wananchi," amesema Ndejembi

Aidha ,Mhe.Ndejembi amewaagiza watendaji hao kusimamia nidhamu ya watumishi kwa kuzingatia sheria za maadili ya utumishi wa umma na kutenda haki wakati wa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi.


Amewasisitiza kuongoza kasi katika  mapambano dhidi ya rushwa kwa kuziba mianya yote ya rushwa ,pamoja na kakusanya mapato ya serikali na kuwasimamia watumishi wenye dhamana ya kukusanya mapato wafanye kazi kwa uaminifu ili kufikia malengo ya serikali.


Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa kikao kazi hicho ambaye pia ni Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Halmashauri ya wilaya ya Rombo, Bi.Judith Mahende amesema kuwa wamepokea mafunzo na maelekezo yote waliyopatiwa katika kikao kazi hicho na watakwenda kuyafanyia kazi kwa ajili ya maslahi ya taifa na wananchikwa ujumla.

"Tumeyapokea mafunzo na maelekezo yote na tutakwenda kuyafanyia kazi katika halmashauri zetu,kwa mfano suala la nidhamu kwa watumishi wa umma,mapambano dhidi ya rushwa na ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya serikali tutahakikisha yanatumika kama ilivyopangwa na kwa wakati,"amesema Mahende

No comments:

Post a Comment