SONGEA YAVUKA MALENGO UKUSANYAJI MAPATO YA NDANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, February 14, 2023

SONGEA YAVUKA MALENGO UKUSANYAJI MAPATO YA NDANI

Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Dkt. Fredrick Sagamiko


Na Ahmed Sagaff, MAELEZO

Manispaa ya Songea imevuka malengo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani katika mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo makusanyo yalifikia asilimia 113.

Ukusanyaji wa fedha hizo umetokana na uadilifu wa viongozi wa manispaa hiyo ambao wanafanya kazi kwa bidii katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2020-2025).

Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Dkt. Fredrick Sagamiko amenukuliwa na Ruvuma TV akitoa takwimu hizo alipokuwa akizungumza na Baraza la Madiwani jana mjini Songea.

“Kwa mwaka wa fedha 2021/2022, kwa upande wa mapato ya ndani tulikisia kukusanya shilingi bilioni 4.3 lakini tulikusanya shilingi bilioni 4.8 ambayo ni sawa na asilimia 113,” ameeleza Dkt. Sagamiko.

No comments:

Post a Comment