Na Ahmed Sagaff, MAELEZO
Viongozi wa dini nchini wameombwa kuongeza juhudi za kutoa elimu ya maadili shuleni ili watoto wajifunze maadili mema yatakayosaidia katika ujenzi wa Taifa.
Akizungumza jana jijini Tanga, Afisa Tarafa wa Pongwe, Ndg. Adelaida Biyengo amesema watoto wanatumia muda mwingi wakiwa shuleni kuliko muda wanaokaa na wazazi wao majumbani.
“Nawaomba masheikh, wachungaji na vikundi vingine waendelee kujisajili ili watoe huduma shuleni, kwasabbu malezi ya mtoto yanaanzia kwetu sisi na ni jukumu letu kama Taifa kuendelea kuwalea watoto wetu,” ameeleza Ndg. Biyengo.
Naye, Muandaaji wa Kongamano la Kutokomeza Maadili Potofu na Kustawisha Taifa kwa Kupanda Miti, Mchungaji Agnes Kipande amesema watoto wakifundishwa maadili ya kupanda miti, Taifa litapunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.
Serikali inaendelea kutekeleza Ibara ya 80 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2020-2025) inayoelekeza kuimarisha masomo ya maadili, uzalendo wa kitaifa na uraia kwa shule zote nchini.
No comments:
Post a Comment