WADAU UNGENI MKONO JUHUDI ZA WANAWAKE NA WASICHANA KWENYE SEKTA YA SAYANSI-KIPANGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, February 11, 2023

WADAU UNGENI MKONO JUHUDI ZA WANAWAKE NA WASICHANA KWENYE SEKTA YA SAYANSI-KIPANGA

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga,akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu yaliyofanyika leo Februari 11,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Prof.Maulilio Kipanyula,,akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu yaliyofanyika leo Februari 11,2023 jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Ushauri na Usaidizi wa Vyuo vya Ufundi Mhandisi Dkt. Gemma Kishari Modu,akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga (hayupo pichani) mara baada ya kuhutubia hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu yaliyofanyika leo Februari 11,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga (hayupo pichani),wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu yaliyofanyika leo Februari 11,2023 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kuhutubia hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi mwaka 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa Sayansi,Teknolojia na ububifu yaliyofanyika leo Februari 11,2023 jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma

Serikali imetoa wito kwa wadau wa sekta za umma na binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za wanasayansi wanawake na wasichana katika kuimarisha mchango wa utafiti na ubunifu wa kisayansi wenye tija kwa ustawi wa uchumi kwa maisha ya kizazi cha leo na kesho.

Hatua hiyo itawezesha kukua kwa sekta zingine ikiwamo viwanda na sekta nyingine za kipaumbele ifikapo mwaka 2025

Akizungumza leo Februari 11,2023 jijini Dodoma, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kimataifa ya siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika Sayansi,Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga amesema kuwa ubunifu unaofanywa na wanawake na wasichana unahitajika na unachangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi kwa taifa.

"Uwekezaji unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika miundombinu na rasilimaliwatu unasaidia kufanyika kwa utafiti wa kisayansi unaolenga kuzalisha bunifu na teknojia zinazojibu changamoto za watanzania," amesema Kipanga

Kipanga amesema maadhimisho hayo yanatumika kama sehemu ya kuwahamasisha wasichana na wanawake kuhamasika kusoma masomo ya sayansi, hisabati,uhandisi na ubunifu ili kuongeza namba za wanawake na wasichana katika soko la ajira kwa upande wa Sayansi.

"Siku hii itumike kuwahamasisha wanawake na wasichana kujikita zaidi kusoma masomo ya sayansi, uandisi,hesabu,ubunifu na teknolojia,"amesisitiza Kipanga

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya afya na masuala ya UKIMWI Mhe.Stanslaus Nyongo (Mb) amesema pamoja na jitihada kubwa za kuwasaidia watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi, bado kuna changamoto ya walimu wa masomo ya sayansi ni wachache.

"Jitihada ni kubwa sana zinazofanywa na Serikali ila bado kuna changamoto kwa upande wa walimu wanaofundisha masomo ya sayansi hivyo ni vyema tukaongeza jitihada katika kuwatengeneza walimu watakaokuja kuwa msaada katika kuwafundisha watoto hawa katika masomo haya ya Sayasi,hesabu,uandisi,na ubunifu,"amesema Nyongo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, teknolojia na ubunifu Prof.Maulilio Kipanyula amesema kuwa, nchi za Afrika ushiriki wa wanawake na wasichana katika masomo ya Sayansi, teknolojia,ubunifu na Hisabati ni asilimia 24 tu,hivyo maadhimisho hayo ni sehemu ya kuwahamasisha wanawake na wasichana kushiriki kikamilifu katika masomo ya Sayansi, teknolojia na ubunifu.

"Maadhimisho haya yanatumika kuhamasisha wanawake na wasichana kushiriki kikamilifu katika masomo ya sayasi,teknolojia,ubunifu na hisabati naamini tukifanya hivi hata huko kwenye soko la ajira wataongezeka,"amesema Kipanyula

No comments:

Post a Comment