Waziri Dkt. Pindi Chana Akaribisha Wawekezaji Sekta za Wizara - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 23, 2023

Waziri Dkt. Pindi Chana Akaribisha Wawekezaji Sekta za Wizara


Na Shamimu Nyaki, Dar-es-salaam 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, amewakaribisha Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mhe. Dkt. Pindi Chana amekaribisha wadau hao leo Februari 23, 2023 jijini Dar es Salaam alipohudhuria utiaji saini mkataba wa ushirikiano katika michezo uliofanyika katika Ubalozi wa Italia hapa nchini kati ya Mwekezaji wa Tan Worrios Sports Academy, Bw. Mainga Kataila na Mwekezaji Riccardo Giacomon wa nchini Italia .
           

Mhe. Pindi Chana ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia Wawekezaji kuwa, Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni nchi ya amani yenye mazingira bora ya uwekezaji.

"Ukitembea na waridi lazima utanukia, sisi kama Serikali tunaamini makubaliano haya yatazaa matunda kwa nchi yetu kwa kuwa tunaamini yataibua na kukuza vipaji vingi.

Kwa upande wake Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lambardi amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Naye Mkurugenzi wa Tan Worrios Sports Academy, Bw. Mainga Kalaita amesema Taasisi hiyo ipo mkoani Morogoro na inakuza vipaji vya mpira wa Soka kuanzia umri wa miaka 5 hadi 22 na inatarajia kuongeza idadi ya vijana.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo, Ally Mayay na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha.

No comments:

Post a Comment