Katika Majadiliano hayo , Waziri Bashe amepokea taarifa ya utekelezaji wa Makubaliano yaliyofanyika Mwaka Jana wa kufufua kiwanda cha Shayiri kilichopo Mkoa wa Kilimanjaro, Ikiwa ni Makengo ya kufikia kutoagiza Shayiri kutoka Nje ya Nchi baada ya Mwaka Mmoja.
Aidha Wizara na TBL wamekubaliana kuzalisha Shayiri kupitia mradi wa Vijana na wanawake wa BBT na Ushiriki wao katika Block Farms system.
Vilevile Waziri Bashe amepokea Taarifa ya mfumo mpya wa kuhudumia wakulima kwa kutumia technolojia ya kisasa ( Block chain Farming System) Mfumo ambao umeshafanyiwa Majaribio Mwaka huu na kufanya Vizuri
Pia Wizara ya Kilimo itashirikiana na TBL kwenye Upande wa ICT, na kufanya kazi kwa karibu na TFRA kwa kutumia mfumo wa Block chain System katika Usambazaji wa Mbolea kwa Wakulima.
No comments:
Post a Comment