Na Okuly Julius-Dodoma
WAZIRI wa Madini Dkt.Dotto Biteko, amemkabidhi majukumu ya kuyafanyia kazi katibu mkuu mpya wa wizara hiyo ikiwemo kuwafanya waajiriwa wa Wizara hiyo kujiona wao ni wa muhimu kutokana na muda mwingi watumishi hao kutumia wakiwa kazini ili kusimamia malengo yaliyowekwa na serikali yakamilike.
Biteko, amebainisha hayo leo Machi,10,2023 jijini Dodoma wakati wa kikao cha kumtambulisha Katibu Kheri Mahimbali, kwa watumishi wa idara zote za wizara ya madini.
Amesema katika wizara hiyo wapo watu wa aina mbalimbali ambao katibu mkuu atakwenda kufanya nao kazi hivyo anapaswa kuwa makini ili kuhakikisha kazi zinafanyika na kufikia malengo ya serikali.
"Ndugu katibu mkuu hapa unaowaona wapo watu wa kila aina wapo ambao ukiwapa kazi wao wanaangalia dead line hata kama kazi uliwapa haijakamilika wanakuletea, lakini wapo ambao kazi hawamazili kwa wakati na wala majibu hawakupi.
"lakini pia wapo ambao wao kazi hawafanyi kabisa, lakini wapo wengine ambao wao ukiwapa kazi wanafanya na ukiwarekebisha wafurahi kurekebishwa lakini wengine ukiwarekebisha wanakukasirikia"amesema Biteko
Aidha, Dkt.Biteko amesema kutokana na muda mwingi watumishi kuutumia wakiwa kazini katibu mkuu anatakiwa kuwafanya waajiriwa hao kujiona wao ni wa muhimu katika wizara hiyo.
"Pili mfanye ambaye hataki kufanya kazi yake aifanye mbinu gani utatumia unazijua vizuri mimi sitaki kukufundisha la tatu mfanye kila mtanzania atamani kufanya kazi wizara ya madini karibu sana wizara ya madini nakutakia kilaraheli"alisema
Naibu waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa, amesema yapo mambo mengi ambayo wameyafanyia kazi hadi sasa ikiwemo kupunguza idai ya watu waliokuwa wamekaimu katika nafasi mbalimbali.
"Katibu mkuu nashukuru kuwa umeeleza kuwa unapaenda kufanya kazi kama timu mie pia ni muumini wa ushirikiswaji lakini toka nimeingia madarakani katika nafasi hii mambo mengi tumeyafanyia kazi ikiwemo kupunguza idadi ya watu waliokua wakikaimu katika nafasi mbalimbali.
"Hivyo tunakuomba katika nafasi ambazo bado hazijafanyiwa kazi uone ni namna gani zinafanyiwa kazi ili maeneo yanayokaimiwa yapate watu na kazi ziendelee kwa malengo tuliyojiwekea"amesema Dk. Kiruswa
Kutokana na timu iliyoundwa kwenye wizara hiyo kazi ndiyo inapaswa kuwa kipimo cha ukarimukatika.
No comments:
Post a Comment