WANAFUNZI 1103 TABORA WANUFAIKA NA ELIMU YA AFYA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 10, 2023

WANAFUNZI 1103 TABORA WANUFAIKA NA ELIMU YA AFYA.


Na Elimu ya Afya kwa Umma

Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kwa kushiriana na Timu ya Uendeshaji wa huduma za Afya ngazi ya Mkoa wa Tabora imeendesha zoezi la kutoa Elimu kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo Elimu kuhusu VVU na Ukimwi, Elimu kuhusu ukatili wa Kijinsia, Elimu Kuhusu Unyanyapaa na mimba za utotoni, Elimu kuhusu Afya ya Akili na Lishe na madhara ya kujihusisha na mapenzi katika Umri mdogo kwa Wanafunzi wa shule za Sekondari za Misha na Bambamzinga zilizopo katika Manispaa ya Tabora .

Elimu imetolewa na kuweza kuwafikia Jumla ya Wanafunzi 1123.
ambapo katika shule ya Sekondari Misha Wanafunzi waliofikiwa ni Wanaume 152 na Wasichana 202 . 


Utoaji wa Elimu hiyo ni utekelezaji wa afua mbalimbali za uelimishaji zinatumiwa na Wizara ya Afya ,Idara ya Kinga Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kwa kushiriana na Ofisi ya Rais Tamisemi pamoja na Timu za Uendeshaji wa huduma za Afya ngazi za Mikoa kwa lengo la kuwafikia Wanafunzi ili kuweza kuwapa Elimu itakayo saidia katika malezi na makuzi yao lakini pia waweze kuchukua hatua za kujikinga dhidi ya Magonjwa mbalimbali , Ukatili pamoja na unyanyasaji wa Kijinsia


Elimu hiyo imetolewa na Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Tabora Dkt.Zubeda Makwaya, Pamoja na Mtaalamu wa Magonjwa ya Akili Dkt.Ndijuye.

No comments:

Post a Comment