Na Okuly Julius-Dodoma
Kanisa la EAGT Tanzania kwa kutambua mchango uliotolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt. Brown Abel Mwakipesile katika utumishi wake, wameamua kununua na kumkabidhi gari kwa ajili ya kuendelea kumrahisishia katika safari za kueneza neno la Mungu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Gari hilo ni sehemu ya shukurani kwa Askofu huyo ambaye amekuwa akijitaabisha kwa kazi ya Mungu kwanzia ngazi ya chini,majimbo mpaka taifa hivyo kutokana na jitihada zake zinazoonekana kwa ustawi wa kanisa hilo na kutambulika kwa kazi anazozifanya ikawapasa kanisa kumnunulia chombo cha usafiri.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa gari hilo leo Machi 8,2023 Jijini Dodoma Dkt.Mwakipesile amesema kuwa alipopata taarifa za kununuliwa gari hilo kwa mara ya kwanza alijiuliza mara nyingi kuwa ni namna gani kanisa hilo wataweza kulinunua gari hilo ila baada ya kukumbuka kuwa hiyo ni kazi ya Mungu na haijawahi kukwama akaamini kuwa ni lazima maono hayo yatatimia.
"Nilipoambiwa kwa mara ya kwanza kuwa nitanunuliwa gari ukweli niliwaza sana kwani najua hali ya uchumi kwa sasa ilivyo ila nikakubaliana tu na mawazo ya watumishi wa Mungu waliokuwa wamebeba maono hayo kwa sababu niliamini ni Mungu ndio anazungumza ndani yao na leo wamenikabidhi na mpaka sasa nakosa maneno ya kusema zaidi ya kusema asante,"
Na kuongeza kuwa "Mkono unaotoa siku zote unabarikiwa sana hivyo pale mlipopagusa kwa namna yeyote kufanikisha kazi ya Mungu naamini mtajazilishwa na baraka za Mungu zitaendelea kumiminika kwenu,"amesema Dkt.Mwakipesile
Dkt.Mwakipesile amesema kwa kupewa gari hilo yeye anaona kuwa ameongezewa mzigo mwingine wa kufika mbali zaidi kuendelea kueneza neno la Mungu.
Katika hatua nyingine Askofu Mkuu huyo amezungumzia siku ya kimataifa ya wanawake duniani ambapo amewataka Wanawake kutambua ratiba ,hasa katika majukumu ya kulea na kutunza watoto pamoja na waume zao kwa sababu mwanamke ndio wenye uchungu zaidi hivyo wanapaswa kuwa na wajibu wenye utaratibu wa kifamilia.
Aidha,Dkt.Mwakipesile amewaasa wanadamu kutopumbazika na utandawazi kwa sababu Misingi ya Mungu ipo wazi na inaelekeza namna Mwanadamu anapaswa kuishi kwa kufuata mienendo ya Biblia.
Hata hivyo, Dkt. Mwakipesile amesema Kanisa la EAGT wanapambana kuubiri injili watu kuacha Uovu wabaki na mawazo waliyopewa na Mungu ili wapate kumuheshimu Mungu anapowapa afya na uzima.
''mambo ya ushonga,ulawiti ni kinyume na mapenzi ya Mungu na yataleta hukumu kubwa kwa wanadamu na hii italeta laana kubwa hata katika familia na jamii watanzania waepuke kuigiza sana vitu visivyofaa''amesema Dkt.Mwakipesile.
Kwa upande wake Makamu Askofu Mkuu (EAGT) Askofu. Joshua Wawa amesema Dkt. Mwakipesile amekuwa akijitaabisha kwa kazi ya Mungu kwanzia ngazi ya chini hadi majimbo hivyo kutokana na jitihada zake na kuzitambua kwa kazi anazozifanya ikawapasa wao kama kanisa kumnunulia chombo cha usafiri.
''Amekuwa akijitaabisha kwa kazi ya Mungu kwanzia ngazi ya chini hadi majimbo na kutokana na jitihada na kuzitambua kazi anazozifanya ikatupasa sisi kumnunulia chombo cha usafiri''amesema Askofu Wawa.
Hata hivyo amehitimisha kwa kusema kanisa imefanya hayo kwa ujulisho kuwa ukitenda vyema kazi ya Mungu utaenziwa kuanzia Duniani.
No comments:
Post a Comment