Na. Asila Twaha, OR- TAMISEMI
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Adolf Ndunguru amekabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Prof. Riziki Shemdoe ambaye sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Makabidhiano hayo yamefanyika Machi 06, 2023 kwenye Ofisi ya Rais iliyopo katika Mji wa Serikali Mtumba na kushuhudiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo.
Aidha, amewashukuru menejimenti kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi chote alichoongoza Wizara hiyo na amewaomba watumishi hao kuendelea kutoa ushirikiano na kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu kwa viongozi hao walioteuliwa lengo likiwa kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake, Katibu, Mkuu Ndugu Adolf Ndunguru amemshukuru Prof. Riziki Shemdoe na kumuahidi kuyaendeleza yote aliyompatia ili wananchi waendelee kuwa na imani na Wizara hiyo na kuwa atafanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na ubunifu.
“Ninakushukuru kwa kunikabidhi ofisi nitaendeleza yale ambayo umeniachia na mbali ya haya yaliyoandikwa humu kwenye vitabu lakini pia nikiwa na jambo la kukuuliza nitakuja mwenye kukuona ili unipe mwongozo zaidi” Ndunguru
Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshuhulikia afya Dkt. Grace Magembe ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya.
No comments:
Post a Comment