MKANDARASI AKABIDHIWA ENEO LA UJENZI WA KITUO CHA TAIFA CHA KUTHIBITI MAAFA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 1, 2023

MKANDARASI AKABIDHIWA ENEO LA UJENZI WA KITUO CHA TAIFA CHA KUTHIBITI MAAFA

Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bi Stella Mwaisaga (kulia) akimkabidhi Ramani ya ujenzi wa Jengo la Ofisi ya kudhibiti Maafa katika eneo la Nzuguni Bw. Juma ambaye ni Mkandarasi wa mradi huo.
Baadhi ya wajumbe wakisikiliza wakati wa hafla hiyo.
Msimamizi Mkuu kutoka kampuni ya Mshauri Elekezi Aru Built Enviromental Consulting Company (ABECC) Bi. Oliva Gonda akionesha Ramani ya Ujenzi wa Jengo hilo.

Na Mwandishi Wetu – Dodoma

Serikali Imekabidhi eneo la ujenzi wa majengo ya kituo cha Taifa cha kudhibiti Maafa kwa Mkandarasi, Kiure Engineering Limet, lilipo Nzunguni Jijini Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, wakati wa Hafla ya makabidhiano ya kituo hicho Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali watu kutoka Ofisi hiyo, Bi Stella Mwaiswaga alisema kuwa, mradi huo wa ujenzi wa kituo hicho utahusisha ujenzi wa majengo ya maghala, awamu ya kwanza unaoendelea kwa sasa, ujenzi wa jengo la ofisi awamu ya pili unatakiwa kuanza na majengo mengine ya uendeshaji yatakayojengwa kulingana na upatikanaji wa fedha.

Bi Mwaiswaga Alibainisha kuwa Ujenzi huu wa awamu ya pili unaotarajiwa kukamilika kwa kipindi cha miezi kumi na mbili, utagharimu kiasi cha shilingi 8,850,000,000 ikiwa ni gharama za mkandarasi zinazojumuisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Awali akiongea katika makabidhiano hayo Mhandisi wa mradi kutoka Ofisi ya waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu Joseph Muhamba alisema lengo la serikali kuwa na kituo hicho nikuwawezesha wafanyakazi wake kufanya kazi katika mzingira wezeshi.

No comments:

Post a Comment