Na. Angela Msimbira, DAR ES SALAAM
SERIKALI imejipanga kuhakikisha tarafa zote za Mkoa wa Dar es Salaam zinakuwa na kituo cha afya ikiwa ni lengo la Rais Samia Suluhu Hassan la kusogeza huduma za afya kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa Machi 1, 2023 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki wakati wa kukagua miundombinu ya afya katika Halmashauri ya Jiji la Dar-es-salaam, Mkoani Dar es Salaam.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameweka mkazo katika Sekkta ya afya kuhakikisha  tarafa zote  zinakuwa na uhakika  wa kuwa na kituo cha afya  kwa Dar es Salaam. 
Kairuki amesema
kwa upande wa kata ya Kinyerezi kupitia Halmashauri ya Jiji, Serikali imetoa takribani Sh. milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa zahanati ya Kinyerezi kwa lengo la kupandisha hadhi zahanati hiyo na kuwa Kituo cha afya na tayari majengo manne yamekamilika ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi. 
Amesema kwa upande wa Kata ya Kimanga,  Serikalli imetenga Sh. milioni 140  kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo.
" Kwa Kata ya Bunyoka tutaanza na wodi ya wazazi pamoja na kliniki ya mama na mtoto lakini kutokana na miinuko tumewaelekeza wananchi kukaa na kushauri kuona kama majengo haya  yajengwe maeneo yaleyale au kupata eneo lingine."
Aidha, Kairuki amesema kuwa Kata ya Kiwalani imepelekewa Sh. milioni 500 na tayari majengo zaidi ya manne yanendelea kujengwa.
Amesema, Kata ya Segerea
tayari Serikali imetenga Sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Segerea na ujenzi unaendelea  kwa jengo la wazazi, maabara, upasuaji, mionzi na kufulia ambapo Sh. milioni 150 zimeongezwa kwa ajili ya kununulia vifaa tiba.
 


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment