ZAIDI YA WATU 200 WAJITOKEZA KUPATA ELIMU YA SURUA KWA NJIA YA SINEMA MIGUNGA KATAVI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, March 9, 2023

ZAIDI YA WATU 200 WAJITOKEZA KUPATA ELIMU YA SURUA KWA NJIA YA SINEMA MIGUNGA KATAVI.


Na.Elimu ya Afya kwa Umma

Elimu ya ugonjwa wa Surua pamoja na uhamasishaji wa chanjo kwa njia ya magari ya matangazo na sinema imeendelea kuzaa matunda baada ya zaidi ya wananchi 200 kutoka kijiji cha Migunga kujitokeza kufuatilia kupata elimu hiyo usiku wa Machi 8.2023.


 
Hatua hiyo ni kutokana na Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Elimu ya Afya kwa Umma kuweka mkazo wa kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uelewa juu ya Surua na umuhimu wa kuwapeleka watoto chanjo.

 
Hivyo, pamekuwa na mwitikio mkubwa wa wananchi kuleta watoto wao kupatiwa chanjo baada ya kupata elimu hiyo ambapo wamekuwa wakiwaleta watoto kupata chanjo huku wakitazama sinema.


No comments:

Post a Comment