Na Okuly Julius -Dodoma
CHUO Kikuu cha Mzumbe kupitia Kitivo chao cha sayansi na teknolojia,
kimesema kitaendelea kuibua,kuendeleza,kutangaza na kuzitafutia masoko bunifu mbalimbali zinazoibuliwa na wanafunzi wa chuo hicho huku kikidai tayari ina kitengo maalum cha kusimamia bunifu hizo.
Chuo kikuu cha Mzumbe kimeshika nafasi ya pili Kwa ubora wa bunifu zao kwenye kundi la Vyuo Vikuu vya Serikali vilivyoshiriki katika maonesho ya Wiki ya ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara ya elimu, sayansi na teknolojia yaliyomalizika APRILI 28,2023.
Akizungumza katika banda la chuo hicho katika maonesho hayo Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha, amesema kuwa katika mambo wanayofanya katika kitivo hicho ni pamoja na wanafunzi kuja na bunifu mbalimbali ambazo zinaenda kutatua changamoto za wananchi.
Prof Mwegoha amesema wanayafurahia maonesho hayo kwani yanahamasisha bunifu mbalimbali pamoja na masuala ya Sayansi na Teknolojia.
Amesema bunifu ambazo wamekuja nazo ni kwa ajili ya kupambana na changamoto za afya,mazingira,usafirishaji na uchukuzi.
“Sasa hivi tuna kitengo maalum kabisa kwa ajili ya kusimamia bunifu,baada ya hapa hawa vijana ili zile waweze kuzitangaza zifike mahali ambako wataweza kutengeneza biashara ambazo zitawainua kiuchumi.
“Hii inaendana na sera ya kitaifa ya kuhakikisha kwamba vijana wanajiajiri vijana wanaokuja hapa wanakuja na mawazo yao na tunawapa ushuri na baadae kuzigeuza kuwa biashara ikiwa ni pamoja na kuwatafutia wafanadhili ambao watazikuza,”amesema Prof Mwegoha
Amesema kupitia kituo hicho cha ubunifu wameanza kwenye kituo atamizi ambacho kinawataalamu kwa ajili ya kukuza idea zao.
Amesema chuo kinakiwezesha kitengo hicho ili kuendeleza miradi na waendelee kuwepo na kuwafikisha katika ndoto zao.
“Tutaendelea kuzisapoti mpaka pale ambapo wanaweza kuziendeleza na kuwa fursa.Hata wakiamua kwenda kufanya hizo kazi wana mahali pa kuanzia,”amesema Prof Mwegoha
Amesema katika bunifu walizokuja nazo ni pamoja na jiko ambalo linatumia mkaa wa taka kwa ajili ya kulinda mazingira.
“Katika bunifu ambazo tumekuja nazo ni jiko ambalo linatumia mkaa wa taka kwa ajili ya nishati na hii ni moja ya bunifu ambazo zipo nyingi ili serikali ikipiga marufuku mkaa tuweze kusapoti, majiko yanatumia taka lakini yanatoa nishati kubwa,”amesema Prof Mwegoha
No comments:
Post a Comment