MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA KAZI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA OSHA KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, April 29, 2023

MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA KAZI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA OSHA KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Mhe, Dkt. Yose Mlyambina akitoa hotuba fupi wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA) mbele ya Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe, Prof. Joyce Ndalichako katika viwanja vya Tumbaku Mkoani Morogoro.


Na Mwandishi wetu- Dodoma

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Mhe. Yose Mlyambina amesema wataendelea kushirikiana na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ili kuhakikisha watumishi wanatekeleza majukumu yao katika hali ya usalama na afya bora.


Ameyasema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe, Prof. Joyce Ndalichako Aprili 28, 2023 katika Uwanja wa Tumbaku Mkoani Morogoro.


Aidha Dkt Mlyambina Amesema wameandaa mkakati wa kupokea elimu kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama na Afya Mahali pa Kazi ambao utahusisha Menejimenti ya Mahakama, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ili kujitathimi na kuzingatia sheria na kanuni za Usalama na Afya mahali pa kazi.


“Katika kuthamini mchango wa OSHA kwa kuheshimu Sheria za Nchi kuhusu umuhimu wa Usalama na Afya mahali pa kazi, mapema mwezi ujao tutatekeleza mkakati huu,” Amesema Dkt. Mlyambina.


Aidha Dkt. Mlyambina amemshukuru Mtendaji Mkuu wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA) kwa kuridhia mpango huo wa utoaji Elimu kwa Menejimenti ya Mahakama Kuu Divisheni ya kazi.

No comments:

Post a Comment