MKUU wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika, Eusebius Mwisongo,akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la Chuo hicho wakati wa Kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Mhadhiri Msaidizi na Mratibu wa maswala ya Udahili Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika,Samuel Marandu,akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda la Chuo hicho wakati wa Kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
WANANCHI mbalimbali wakiendelea kupata elimu katika banda la Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika,walipotembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika Dr.Tumaini Katunzi akisaini kitabu Cha wageni katika Banda la Chuo hicho wakati wa Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
WANAFUNZI wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembela banda la Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika,wakati wa Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
WASHIRIKI kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la Chuo hicho mara baada ya kumalizika kwa Kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Na.Alex Sonna-DODOMA
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika, Eusebius Mwisongo amesema wamebuni mifumo itakayomsaidia mwananchi kufanya shughuli zake kiurahisi ili kuwa na mafanikio kwa haraka.
Hayo ameyasema Aprili 28,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Chuo hicho katika Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yanayofanyika uwanja wa Jamhuri Dodoma
Bw.Mwisongo amesema kuwa lengo ni kuujulisha umma umuhimu na faida za mifumo ya TEHAMA inayotengenezwa chuoni hapo.
“Tumekuja na mifumo sita ambayo inahusu ufatiliaji wa magari, mkulima, kufatilia mahudhulio ya wanafunzi na pamoja na mfumo wa vikoba”, amesema Mwisongo.
Ameitaja mifumo hiyo ni pamoja na E- Task Management,Vehicle Management System, e-mkulima,Class Tracking Attendance System, e-management
Ameeleza kuwa Mifumo hiyo inafanya kazi tofauti kulingana na mahitaji ya mteja mfano kwa taasisi za elimu kuna mfumo wa class tracking attendance ambao huonyesha idadi ya wanafunzi walio hudhulia kipindi husika pamoja na mwalimu.
Lakini ameongeza kuwa wana mfumo wa e- task manengment ambao unawezesha mkuu wa kitengo kupanga majukumu kwa watu wake na wahusika hupata ujumbe wa majukumu waliopangiwa na kutekeleza majukumu yao na kuleta taarfa kupitia mfumo huo.
Hivyo ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao hili kujua ni mafunzo gani wanatoa na huduma zinazopatikana katika banda lao hususani mifumo katika kuendesha shughuli za kijamii.
No comments:
Post a Comment