Na Okuly Julius-Dodoma
Wiki ya Ubunifu Tanzania ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya
kuongeza hamasa ya matumizi ya sayansi, teknolojia na
ubunifu kama nyenzo ya kurahisisha maendeleo ya kiuchumi
na kijamii.
Prof.Mkenda ameyasema hayo leo Aprili 20,2023 Jijini Dodoma,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi yanayoendelea kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya Ubunifu Tanzania yatakayofanyika kuanzia tarehe 24 hadi tarehe 28 mwezi Aprili mwaka 2023 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
"mikakati ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia suluhu Hassan ni kuongeza hamasa ya matumizi ya sayansi, teknolojia na
ubunifu kama nyenzo ya kurahisisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii,"
Na kuongeza kuwa "Tangu mwaka 2019, Wizara kwa kushirikiana na Wadau imekuwa ikiendesha Wiki ya Ubunifu na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) kwa lengo la kuimarisha Mfumo wa Ubunifu nchini,"amesema Prof Mkenda
Prof.Mkenda amesema kuwa Wiki ya Ubunifu pamoja na mambo mengine, imekuwa ikiibua,kutambua na kuendeleza jitihada zinazofanywa na wabunifu na wagunduzi wakitanzania ,hivyo kupitia maadhimisho hayo wabunifu na wagunduzi wanapata fursa ya kuonesha bidhaa zao na hivyo kujulikana kwa wawekezaji, na watumiaji wa bidhaa hizo.
Waziri huyo amebainisha kuwa wiki ya Ubunifu Tanzania inafanyika ili kutoa fursa kwa wabunifu, wagunduzi, watafiti, watunga sera, wadau wa maendeleo na washirika wengine kukutanana na kujadili Sera,Kanuni na Miongozo mbalimbali kuhusu maendeleo ya sayansi,teknolojia na ubunifu.
"Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu mwaka huu yatahusisha,pamoja na mambo mengine; Maonesho ya ubunifu na teknolojia kutoka Taasisi za Elimu ya Juu, Taasisi za Utafiti na Maendeleo, Mashirika na Makampuni ya Umma na Binafsi Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), na Shule za Sekondari na Msingi,"ameeleza Prof.Mkenda
Pia amebainisha kuwa kutakuwa na siku maalum kwa ajili ya kuonesha shughuli zinazofanywa na VETA na ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa lengo la kutoa Elimu kuhusu shughuli za Taasisi hizo kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Prof.Mkenda amesema amesema kuwa ili kuhakikisha Wiki ya Ubunifu Tanzania inawagusa wabunifu katika ngazi zote itatanguliwa na maadhimisho katika ngazi za mikoa na Halmashauri na itaratibiwa na kuendeshwa kwa ushirikiano kati ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Programu ya FUNGUO chini ya UNDP, OR-TAMISEMI na wadau wengine nchini. Aidha maadhimisho hayo yatafanyika kabla ya kuanza shughuli za kilele, tarehe 24 Aprili 2023.
" Mikoa 17 itakayofanya maadhimisho hayo ni pamoja na: Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Iringa, Morogoro, Tanga, Arusha, Mwanza, Kigoma, Kagera, Mara, Ifakara, Njombe, Mtwara, Kilimanjaro, Songwe na Unguja Magharibi kupitia kumbi mbalimbali za ubunifu,"amefafanua Prof.Mkenda
Washiriki wa Maonesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania mwaka 2023 itakayobebwa na kaulimbiu isemayo ‘Ubunifu kwa Uchumi Shindani’ ni Taasisi za Elimu ya Juu, Taasisi za Utafiti na Maendeleo, Vyuo vya Ufundi, Mashirika na Taasisi za Umma, Mashirika na Taasisi binafsi za teknolojia, Wizara mbalimbali na Wabunifu walioendeleza katika programu ya MAKISATU na kufikia hatua ya ubiasharishaji.
No comments:
Post a Comment