SERIKALI YAMWAGA AJIRA 21,200 KATIKA KADA YA AFYA NA ELIMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 12, 2023

SERIKALI YAMWAGA AJIRA 21,200 KATIKA KADA YA AFYA NA ELIMU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah J. Kairuki akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu tangazo la nafasi za ajira kwa kada ya Afya na Elimu, leo tarehe 12 Aprili 2023 Jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa Kada za ualimu na Afya.


Hayo yameelezwa leo Aprili 12, 2023 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jijini Dodoma.


Amesema Idadi ya watumishi watakaoajiliwa katika Kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika shule za Msingi a Sekondari.


Aidha, Waziri Kairuki ameeleza kuwa idadi ya watumishi watakoajiriwa katika kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati.


Waziri Kairuki amesema waombaji wanatakiwa kuomba ajira kuanzia leo April 12, hadi 25,2023 saa 5:59 usiku.


”Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama zifuatazo awe mtanzania,awe na ukomo wa umri miaka 45 cheti Cha taaluma,cheti Cha kidato Cha sita na kitambulisho Cha NIDA.”amesema Waziri Kairuki


Waziri Kairuki amewataka waombaji waliowahi kutuma maombi ya ajira kupitia mfumo wa maombi ya ajira kuhuisha taarifa zao kwenye mfumo wa ajira kupitia kiunganishi ajira.tamisemi.go.tz kwa kutumia namba ya mtihani wa kidato cha nne na nywila au kuomba upya .


Amewataka waombaji wa ajira hizo kuwa tayari kufanyakazi kwenye Halmashauri na vituo watakavyopangiwa, kufanyakazi na mashirika au taasisi zilizoingia ubia na Serikali na baada ya kupangiwa kituo cha kazi hakutakuwa na nafasi ya kubadilishiwa kituo cha kazi 


Aidha ametoa rai kwa waombaji wa ajira hizo kupeuka matapeli watakaowapigia simu na kuwataka kutoa fedha kwa ajili ya kupata ajira kwa kuwa ajira hizo ni bure, vigezo na masharti vitatumika katika kuwaajiri watumishi hao


“Natoa rai kwa waombaji, mtu asije akapigiwa simu kuombwa fedha kwa ajili ya kupata ajira hizo, msiingie katika huo mtego kwa kuwa ikibainika hilo limejitikeza toeni taarifa kwa Mamlaka ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya matapeli” amesisitiza Waziri Kairuki.

No comments:

Post a Comment