
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati wa Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi”, lililofanyika katika Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.

Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba akizungumza wakati wa Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi”, lililofanyika katika Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma, (PPRA), Bw. Dennis Simba, akizungumza wakati wa Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi”, lililofanyika katika Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na Mkurugenzi wa PPRA, Bw. Dennis Simba wakiteta jambo kabla ya ufunguzi wa Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi” lililofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, akizungumza na Maafisa Ugavi wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha alipotembelea Banda la Wizara hiyo kabla ya ufunguzi wa Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi” lililofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.

Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba akimpokea Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, kabla ya ufunguzi wa Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi”, lililofanyika katika Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.

Kutoka kushoto ni Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Dkt. Frederick Mwakibinga, Afisa Ugavi Mwandamizi, Bi. Jamila Byekwaso, Kamishna Msaidizi, Bw. Alex Haraba, Bi. Beatrice Zenda, Bw. Raphael Chima, Bi. Vaileth Mwakajisi na Bi. Beatrice Zenda kutoka Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma na Mkurugenzi wa Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi, Bw. Boaz Ntembanda kutoka Wizara ya Fedha wakati wa Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi” lililofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.

Maafisa Ugavi kutoka Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi” lililofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha)
Na. Eva Ngowi, na Chedaiwe Msuya – WF Arusha
Taasisi nunuzi zote nchini zimeelekezwa kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia matumizi sahihi ya mifumo ya kidijitali katika ununuzi wa huduma nchini, kutenga asilimia za ununuzi wao wa mwaka kwa ajili ya kampuni za mazao na makundi maalumu na kuhakikisha zabuni zilizotengwa kwa wazawa zinatolewa kwa wazawa kama ilivyokusudiwa.
Maelekezo hayo yametolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Doroth Gwajima (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la mwaka 2025, lenya kauli mbiu “Ununuzi wa Umma kidijitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za wazawa na makundi maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi”, linalofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.
Alisema kuwa ni vyema Taasisi nunuzi kuhakikisha kuwa Halmashauri zote nchini zisaidiwe kuibua makundi yote maalumu ya kijamii katika maeneo yao ambayo yatajipatia fursa zilizotengwa na Serikali, kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa ufanisi, pia kuhakikisha Wataalamu wanaohusika katika Taasisi za Ununuzi wa Umma wanazingatia weledi wa taaluma zao na maadili.
Aliiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi Serikalini (PPRA), ihakikishe wanasimamia malengo ya uanzishaji wao kama yalivyowekwa kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura na 410.
Aliwaasa washiriki wote kuzidisha uzalendo kwa kuhakikisha wanazingatia sheria na miongozo ya Serikali na kuonesha kiwango cha juu cha maadili.
Akizungumza katika ufunguzi wa Kongamo hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba aliahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Mhe. Dkt. Gwajima (Mb), kuhusuana na kutoa elimu ya Mfumo wa NEST kwa maafisa maendeleo ya jamii.
“Mhe. Mgeni rasmi ulipokuwa unatembelea mabanda ya maonesho ulitoa maelekezo ya kutoa elimu ya Mfumo wa NEST kwa maafisa maendeleo ya jamii na mwakilishi wa Wizara yako amelieleza kwa ufasaha. Nami nakuhakikishia Mhe. Waziri kwamba sisi Wizara ya Fedha tumepokea hayo maelekezo yako na tuko tayari kwa utekelezaji wa utoaji wa elimu hiyo.” Alisema Dkt. Mwamba.
Vile vile Dk. Mwamba alizishukuru kwa dhati Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma – PPRA, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu na Wizara ya Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu pamoja na watendaji wote wa Wizara ya Fedha kwa maandalizi mazuri ya kongamano hili.
No comments:
Post a Comment