WAHAMIAJI HARAMU 3,110 WALIOMALIZA VIFUNGO VYAO WANAIGHARIMU SERIKALI BILIONI 5.68 KWA MWAKA-CAG - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, April 6, 2023

WAHAMIAJI HARAMU 3,110 WALIOMALIZA VIFUNGO VYAO WANAIGHARIMU SERIKALI BILIONI 5.68 KWA MWAKA-CAG


Na Okuly Julius-Dodoma

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amesema Ofisi yake imebaini kuwa Idara ya Jeshi la Magereza ina wahamiaji 4,419 haramu kutoka nchi mbalimbali, huku 1,264 wakiendelea kutumikia vifungo, 45 wamewekwa mahabusu na 3,110 wanaotakiwa kurejeshwa makwao.


Kichere amebainisha hayo Aprili 6,2023 Jijini Dodoma, wakati akiwasilisha ripoti ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kuhusu ukaguzi wa Serikali Kuu kwa Mwaka wa fedha ulioishiaJuni 30,2022.


Ambapo Kichere amesema uwepo wa wafungwa hao waliomaliza vifungo vyao lakini bado wako gerezani katika kipindi cha mwaka mmoja hadi mitano unatokana na kutokutolewa amri ya kuachiliwa huru na Wizara ya Mambo ya Ndani.


Kichere ameongeza kuwa gharama za kuwahudumia wahamiaji hao ni kubwa, huku Chakula cha mfungwa mmoja kilitengewa bajeti ya Sh. 5,000 kwa siku.


" Kitendo cha kuwa na wahamiaji 3,110 katika magereza hayo huigharimu Sh. bilioni 5.68 kwa mwaka; hivyo kuipa mzigo serikali,"amesema Kichere


Amesema kuwa Idara ya Jeshi la Magereza imeitaka Idara ya Uhamiaji kuchukua hatuastahiki za kuwarejesha makwao wahamiaji haramu wanaomaliza vifungo vyao ili kuepuka gharama za ziada. Waziri wa Mambo ya Ndani ametoa maagizo ya kuzuiliwa ili kuwabakisha wafungwa wa kigeni wanaohitaji kurejeshwa makwao. Hata hivyo, kuwafukuza wahamiaji haramu ni suala la
kidiplomasia linalohitaji mashauriano na Mabalozi wa nje ya nchi.


"Natoa wito kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ikishirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kufanya juhudi zaidi kuhakikisha kwamba maagizo yanatolewa kikamilifu ili kuwarejesha raia wa kigeni walioachiliwa huru nchini kwao na kutatua suala hili kwa ukamilifu wake, na hivyo kupunguza gharama zisizo za lazima,"amesema Kichere


Katika hatua nyingine Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesebu za Serikali Charles Kichere ametoa wito kwa Idara ya menejimenti ya Jeshi la Magereza kuimarisha utaratibu wa kurekebisha tabia ya wafungwa na kuanzisha mipango ya motisha ambayo inaweza kuwa njia bora ya kushughulikia tatizo la kurudia vifungo.


Ambapo ripoti ya Magereza ya mwaka 2021/22 imebainisha kuwa wafungwa 3,252 wamerudishwa gerezani tena katika kipindi cha mwaka mmoja,wafungwa 2,320 wamerudishwa gerezani tena kwa mara ya pili na wafungwa 932 wamerudishwa tena kwa mara ya tatu.


"Kwa kurudia vifungo kwa wafungwa hii inamaanisha kuna kuwepo na gharama kubwa ya kuwatunza hao wafungwa jambo linaloiweka Serikali katika matumizi makubwa ya rasilimali,"amesema Kichere


Kichere amesema kuwa Programu za kurekebisha tabia zinapaswa kuzingatia ujuzi wa ufundi pamoja na kushughulikia sababu za msingi za tabia ya uhalifu kwa wafungwa,kama vile uraibu wa dawa za kulevya au afya ya akili.


"Mipango ya kuwapa motisha wafungwa inaweza kuwahamasisha kushiriki katika urekebishaji wa tabia na kuwapa msaada wanaohitaji ili waweze kufanikiwa kuingia tena katika jamii,"amesisitiza Kichere

No comments:

Post a Comment