BALOZI WA CANADA NCHINI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA THBUB - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 26, 2023

BALOZI WA CANADA NCHINI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA THBUB


Na Mwandishi wetu -Dodoma


BALOZI wa Canada nchini Tanzania, Mheshimiwa Kyle Nunas Mei 25, 2023 ametembelea Makao Makuu ya Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), jijini Dodoma na kufanya na mazungumzo na Mwenyekiti wa Tume.


Lengo la ziara hiyo lilikuwa kujitambulisha kwa uongozi wa Tume, kujua masuala mbalimbali ya utendaji kazi wa Tume na kujadiliana kuhusu maeneo mbalimbali ya mashirikiano katika kukuza na kulinda haki za binadamu na utawala bora nchini.



Katika ziara yake hiyo Mhe. Balozi Nunas aliambatana na Mshauri wake wa masuala ya siasa, uchumi, na mambo ya umma, Bi. Sandra Rossister na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi.Salma Rajab Barak



Katika mazungumzo yao yaliyowashirikisha Makamishna na viongozi Waandamizi wa Tume, Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji Mstaafu) pamoja na mambo mengine alielezea majukumu ya taasisi yake na namna Tume ilivyoshiriki katika uwasilishaji wa taarifa zake za tathimini ya hali ya haki za binadamu nchini (UPR) kwa mizunguko yote mitatu – 2011, 2016 na 2021, na namna inavyoshiriki katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa.

No comments:

Post a Comment