DKT.MOLLEL :MSISIKILIZE KELELE FANYENI KAZI NYINYI NI MBONI YA TAIFA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 3, 2023

DKT.MOLLEL :MSISIKILIZE KELELE FANYENI KAZI NYINYI NI MBONI YA TAIFA.



Na Okuly Julius-Dodoma

Naibu Waziri, Wizara ya Afya Dkt.Godwin Mollel amewataka watumishi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi bila kukatishwa tamaa na kelele za nje ili kuendelea kutoa huduma bora kwa watanzania.


Dkt.Mollel ameyasema hayo leo Mei 3,2023 alipotembelea ba kufanya Mkutano na uongozi pamoja na wafanyakazi wa Hospitali hiyo, ambapo mewakumbusha kuwa serikali inaichukulia hospitali hiyo kama mboni ya Jicho kwa taifa na hiyo inasababishwa na utendaji kazi mzuri wanaofanya.


Pia amewataka kuwapeleka Wauguzi wengi kusoma kwa ngazi ya ubingwa kwani wao ndio wanafanya kazi kubwa ya kuwahudimia wagonjwa baada ya madaktari kukamilisha taratibu zao.


"Madaktari wakumbatieni wauguzi na nielekeze tu kuwa muwapeleke nao wakasome mpaka ngazi ya ubingwa kwa sababu hospitali nyingi wanawasomesha madaktari wengi kuliko wauguzi wakati wao ndio watendaji kazi wakubwa,"amesema Dkt.Mollel


"Naitazama hospitali ya Benjamin Mkapa kwa jicho la kitaifa sio Kikanda kwani lengo ni kuhakikisha huduma zote zinatolewa hapa na ndio maana kwa sasa nchi za jirani zinategemea matibabu kutoka kwetu na sio kusafiri tena kwenda India na nchi zinginezo,"amesema Dkt.Mollel



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Dkt.Alphonce Chandika amesema tangu walipoanza huduma za ubingwa bobezi mwaka 2018-2023 takwimu zinaonesha kuwa wagonjwa waliopandikwa figo ni 33,upande wa wagonjwa wa Moyo Chandika amesema tangu mwaka 2019-2023 wagonjwa waliofanyiwa uchunguzi wa mishipa ya Moyo 796,waliopandikizwa Betri ni 13,watoto waliozibwa matundu kwenye Moyo ni 6 na kuweka vizibua njia ya mishipa ya Moyo (stents) 66.


"Wagonjwa 105 wamepandikizwa vipandikizi kwenye magoti na nyonga tangu mwaka 2021 -2023 na upande wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu 2020-2023 ,upasuaji wa jumla ni 1,186,upasuaji wa ubongo ni 668 na upasuaji wa uti wa mgongo ni 518,"amesema Dkt.Chandika




Katika taarifa yake fupi kwa Naibu Waziri huyo ,Dkt.Chandika amesema kuwa idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa inaongezeka kila mwaka ambapo 2020 wagonjwa waliyohudumiwa ni 143,795, na 2021 ni 195,876 na mwaka 2022 walihudumiwa wagonjwa 234,237 na kwa sasa wakiwa na jumla ya watumishi 963 kati yao 569 ni watumishi wakudumu na watumishi 326 ni watumishi wa Mkataba na kujitolea.


"Pia ameainisha miradi iliyogharamiwana serikali ya awamu ya sita ni pamoja na Mtambo wa kuzalisha hewa tiba ya Oksijeni iliyogharimu bilioni 1.1,Nyumba 40 za watumishi (nyumba hizi zipo katika mradi wa Bilioni 3.01 wa NHC Iyumbu),uanzishwaji wa huduma ya upandikizaji Uloto kwa gharama ya bilioni 1 na ununuzi wa gari lawatumishi milioni 220,amesema Dkt.Chandika


Dkt.Chandika ameongeza kuwa ongezeko hilo la wagonjwa kila mwaka ni kutokana na huduma bora inayotolewa katika hospitali hiyo ambapo hilo lonaendelea kudhiirishwa katika daftari la kuratibu malalamiko na pongezi tangu Januari hadi machi 2023 wamepokea pongezi 5296 sawa na asilimia 99.4 na malalamiko 30 sawa na asilimia 0.6.

No comments:

Post a Comment