DKT.SAMIA : MCHAKATO WA SERIKALI KUHAMIA DODOMA ULIKUWA WA AWAMU ZOTE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 20, 2023

DKT.SAMIA : MCHAKATO WA SERIKALI KUHAMIA DODOMA ULIKUWA WA AWAMU ZOTE.



Na Okuly Julius-Dodoma

Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kukamilika Kwa Ujenzi wa Ofisi ya Rais Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma ni mchakato uliofanyika katika awamu zote Tanzania.


Ameyasema hayo Leo Mei 20,2023 wakati akizindua Jengo la Ofisi ya Rais Ikulu Chamwino,Jijini Dodoma.





"Hii ni Ikulu ya Watanzania na tunajivunia Kwa sababu ni nguvu ya watanzania kwani imejengwa na watanzania wenyewe,"amesema Dkt.Samia



Mchakato wa Kuhamia Dodoma ulianza mapema na umepitia katika ngazi mbalimbali tangu mwaka 1966 ambapo Joseph Nyerere Mdogo wake na Rais wa Awamu ya Kwanza Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere alipopeleke hoja Bungeni la kutaka Dodoma kuwa makao makuu na hoja yake ilipingwa.






Awamu zote zilianza kujenga Ofisi mbalimbali za Serikali na Taasisi zake ambapo katika awamu ya Tano ndipo Msukumo ulipoongezeka.


Mhe.Dkt.Samia ameahidi kuwa atahakikisha Miradi yote iliyokuwa imeanza kutekelezwa na Dkt.Magufuli yatakamilika huku akisema huo ni mradi wa pili kukamilika baada ya uwa Wa Daraja la Tanzanite.


"Kukamilika Kwa Ujenzi wa Ikulu hii ni ishara kuwa sasa Serikali imehamia Dodoma Kwa maana hiyo Dar es Salaam itakuwa tunakwenda tu kupokea wageni wetu wa Kimataifa na tukikamilisha Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato wageni wote tutakuwa tunawapokea hapa hapa na Dar es salaam tutaiacha kama Mji wa Kibiashara,"amesema Dkt.Samia




Akizungumza Kwa niaba ya   Marais Wastaafu, Dkt.Jakaya Kikwete amesema historia ya Tanzania Leo imeandikwa Kwa kalamu ya dhahabu na Ile ndoto ya Rais kuhamia Dodoma Moja Kwa Moja sasa imekamilika.



"Watu wengi walisema Chamwino Sio Dodoma niliwashangaa sana ila Kwa sasa wote wanaijua Chamwino kuwa ipo Dodoma,",amesema Dkt.Kikwete


Amesema kuwa katika kipindi Cha Uongozi wake aliamua Ikulu kujengwa Chamwino na Ofisi za Wizara kujengwa karibu karibu na alipokuja Hayati Dkt.John Pombe Magufuli akatekeleleza Kwa Vitendo ndipo Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino ilipoanza kujengwa na Ofisi za Wizara nazo zimejengwa sio mbali kutoka Ikulu ilipo.


Jengo la Ofisi ya Rais Ikulu Chamwino Jijini Dodoma limejengwa Kwa ushirikiano na Ofisi ya Rais Ikulu,SUMA JKT na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), hivyo Ujenzi huo waliohusika kujenga ni Watanzania wenyewe.


No comments:

Post a Comment