DUWASA,DOHWA WASAINI MKATABA WA UJENZI WA MRADI UONDOSHAJI MAJITAKA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, May 9, 2023

DUWASA,DOHWA WASAINI MKATABA WA UJENZI WA MRADI UONDOSHAJI MAJITAKA


Na Okuly Julius-Dodoma 

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) ,Leo Mei 9,2023 imesaini MKATABA wa Usanifu na Usimamizi wa Ujenzi wa Mradi wa kuboresha huduma ya Uondoshaji na kutibu MAJITAKA na Kampuni ya DOHWA Kutoka Nchini Korea ya Kusaini.


Akizungumza baada ya kushuhudia Utiaji saini huo , Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa majitaka yasipowekewa utaratibu mzuri inaingia katika eneo zima la uchafuzi wa Mazingira.


"Tunaambiwa kuwa Asilimia 80 ya Majisafi yanayotumika na binadamu katika matumizi yake ya kila siku hugeuka kuwa Majitaka sasa tujiulize yanakwenda wapi zaidi ya kwenda kuchafua Mazingira?,"amesema Aweso


Mhe.Aweso amesema kuwa asilimia ishirini (20) pekee ya wakazi wa Dodoma wanapata huduma ya uondoshaji majitaka katika kata 14 kati ya 41 kupitia mtandao wa DUWASA uliopo, ambao ufanisi 
wake hauendani na ongezeko la kasi la watu katika Jiji la Dodoma na uzalishaji wa Majitaka.


Hata hivyo Aweso amekiri kuwa Wizara ya Maji hawajafanya uwekezaji wa kutosha katika eneo la uondoshaji wa Majitaki.


Awali Wakati akitoa taarifa ya Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph amesema kuwa gharama za mradi huo kwenye Usanifu na Ujenzi unategemea kugharimu kiasi cha Dola za Marekani Milioni 70 sawa na Shilingi Bilioni 164.85 za Kitanzania.


Ambapo Mhandisi Aron amesema ,Mkataba wa Usanifu na Usimamizi wa Ujenzi wa Mradi huo utagharimu kiasi cha Dola za Marekani 5,225,000 sawa na takribani Shilingi Bilioni 12.3



"Mradi huu unalenga kuhusisha Usanifu na ujenzi wa Mabwawa mapya makubwa 16 yenye uwezo wa kutibu takribani lita milioni 20 kwa siku,usanifu na ujenzi wa bomba kubwa (trunk main) kwa kilometer 107.5,ubadilishaji wa bomba chakavu kilomita 2.6 na ukarabati wa Kilomota 2.1 za Mtandao wa majitaka,"amesema Mhandisi Aron


Aidha ,Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha Miezi 49 kutoka tarehe ya leo ambapo awamu ya kwanza Mhandisi Mshauri atafanya kwa muda wa miezi 13 kusanifu Mradi na awamu ya atatumia miezi 36 katika ujenzi wa Mradi huo.

No comments:

Post a Comment