Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini Hali ya Uchumi ya Vyombo vya Habari na wanahabari Ndg.Tido Mhando akizungumza na Waandishi wa habari pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo,Leo Mei 23,2023 Jijini Dodoma. |
Na Okuly Julius-Dodoma
Awali Kamati hiyo ilipewa Muda wa Miezi mitatu kukamilisha ripoti yake ila baada ya kuwashirikisha wataalamu kutoka Vyuo Vikuu na TCRA na kupata tathmini ya kitaalamu ndipo wakabaini kuwa kazi hiyo ni kubwa tafouti na walivyokuwa wanafikiria.
Akizungumza na vyombo vya Habari , leo Mei 23,2023,Jijini Dodoma, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye ,amesema kuwa kazi ya Kamati hiyo ni kubwa hivyo inahitaji umakini katika utekelezaji wake kwani ndio imebeba hatma ya Vyombo vya Habari na Waandishi wa habari.
"Ni matumaini yangu kuwa Kamati hii itatumia vyema Miezi hii sita kufanya tathmini na kuja na ripoti kamili itakayokuwa imebeba maslahi ya Vyombo vya Habari na wanatasnia na Mhe.Rais Dkt.Samia anasubiria sana ripoti yenu hivyo mkae mkijua kuwa taifa zima lipo kimya kusubiria mtakuja na kipi,"amesema Mhe.Nape
Mhe.Nape ametoa wito Kwa Wamiliki wa Vyombo vya Habari,Wanahabari na Wadau wa Habari hapa nchini kutoa ushirikiano Kwa Kamati hiyo na penye kuhitaji ushauri waishauri Kamati hiyo ili kuisaidia kukamilisha kazi yake Kwa ufanisi.
"Nitoe wito Kwa Wanahabari na Wadau wa habari kuiunga mkono hii Kamati penye kuhitaji kushauri washaurini kama Kuna kosa sehemu waambieni ili kuja na ripoti iliyokamilika Kwa maslahi ya Tasnia ya habari nchini.
Pia Mhe.Nape amesema kupitia Wizara yake itasimamia madeni yote yanayodaiwa na Vyombo vya Habari Serikalini na kwenye Taasisi zinalipwa hata kama sio Kwa pamoja ila waanze kulipwa kidogokidogo iwezekanavyo.
"Tunapozungumzia Ustawi wa Vyombo vya Habari nchini huwezi kuacha kugusia Madeni yaliyopo Serikali na kwenye Taasisi kwani Fedha hizo ndio zinazotakiwa kutatua changamoto zinazoikabili hivyo nitahakikisha pesa hizo zinalipwa hata kidogokidogo,"Amesema Mhe.Nape
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndg.Tido Mhando amesema kuwa watafanya kazi hiyo Kwa umakini bila kukurupuka kwani Serikali inasubiri taarifa kamili ili kuepukana na kutoa taarifa ambayo haijajitosheleza.
"Tumekaa tukatathimini na kubaini kwamba Muda tulikuwa tumepewa ni mdogo sana ukilinganisha na uzito wa jambo lenyewe ambalo linatakiwa kuja na majibu yaliyojitosheleza kwani sisi tumebeba Maslahi ya Tasnia ya Habari,
Na kuongeza kuwa "Mimi na wanakamati wenzangu tumeomba kuongezewa Muda mpaka Mwezi Novemba 2023 na tunaishukuru Serikali kupitia Wizara ya Habari kwa kuridhia ombi hilo baada ya kuona ukubwa wa kazi hii na sisi tutahakikisha tunautumia kukamilisha kazi hii,"amesema Tido
No comments:
Post a Comment