MHE.SAGINI:WAFANYAKAZI MSISAHAU JUKUMU LA MSINGI LA MALEZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 1, 2023

MHE.SAGINI:WAFANYAKAZI MSISAHAU JUKUMU LA MSINGI LA MALEZI


Na Okuly Julius -Dodoma

Naibu Waziri ,Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Mhe.Jumanne Sagini ametoa wito kwa Wafanyakazi wote, mbali na kazi zao za msingi za kila siku wanazozifanya kutosahau kuungana kwa pamoja katika malezi ya watoto na kusimamia maadili mazuri ili kutengeneza kizazi kizuri kwa ujenzi wa taifa.


Mhe.Sagini ametoa Wito huo leo Mei 1,2023 Jijini Dodoma ,wakati akizungumza Katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.



"Najua tuna kazi nyingi ila tusisahau jukumu letu la msingi la malezi hili haliepukiki na tukizembea haya tutatengeneza kizazi ambacho hakitakuja kusaidia jamii wala taifa kwa miaka ijayo,"Amesema Mhe.Sagini



Pia Sagini amewataka waajiri kuhakikisha wanawasilisha michango ya waajiriwa wao kwenye mifuko ya uhifadhi wa jamii kwani kutokufanya hivyo wanawanyima haki ya msingi waajiriwa wao na kusababisha misuguano yanapotokea matatizo.



"Na nyie Mifuko ya jamii msikae kimya kwa waajiri ambao hawapeleki michango na msisubiri mpaka mtumishi atakapostaafu au  afariki ndio muanze kufuatilia kwa sababu sio sawa shughulikieni haya mapema ili kuepuka na minong'ono,"amesisitiza Mhe.Sagini



Aidha amewataka waajiri kuacha tabia ya kuwachagulia wafanyakazi vyama vya wafanyakazi vya kujiunga navyo kwani kufanya hivyo ni kuwanyima uhuru wao kwani kila mfanyakazi ana uhuru wa kuchagua ni Chama gani ajiunge nacho.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Wizara ya Habari, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Suleiman Mvunye amesema kuwa wafanyakazi wanapaswa kutambua umuhimu wa siku hii kwani inawapa nafasi ya kuwasilisha maoni yao kwa serikali kupitia vyama vyao.


Pia amezungumzia Mradi wa Anuani za Makazi kuwa ni mradi ambao umesaidia kuunganisha nchi nzima na kurahisisha upokeaji na utoaji wa huduma pamoja na masuala ya ulinzi na usalama.


"Leo hii ikitokea nyumba imeungua eneo lolote inakuwa rahisi kufikiwa kwa sababu mradi wa anuani za makazi umerahisish la ufikiaji wa maeneo mbalimbali,"amesema Mvunye


Naye Innocent Jacob ambaye no Mtaalamu wa anwani za makazi amesema kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya watanzania wanajua kutofautisha anuani za makazi na Postikodi hivyo kurahisisha huduma mbalimbali na kuepukana na maelekezo mengi kama huko awali.


"Zamani ukitaka kufuka eneo fulani mtu anaweza kukuelekeza kwa kukuambia labda mbele utakuta mti mkubwa sehemu fulani sasa je,ukifika ule mti ukiwa tayari umeshakatwa itakuaje zaidi ya kupotea ndio hapa tunaona umuhimu wa Mradi huu wa Anuani za makazi,"amesema Jacob

No comments:

Post a Comment